Gregory Damons (alizaliwa 13 Juni 1995) ni mchezaji wa soka anayecheza kama beki kwa timu ya Moroka Swallows kwenye ligi kuu ya Afrika Kusini.

Maisha ya awali hariri

Gregory Damons alizaliwa huko Gelandale Port Elizabeth, akiwa mtoto mdogo wa watoto wawili. Alisoma katika shule ya Sekondari ya Gelandale na baadae alisoma shule ya Western Cape Sports baada ya kupewa ufadhili kutokana na kucheza katika Mashindano ya Engen Knockout Challenge. Baada ya kuondoka shuleni,alifanya kazi katika mapokezi ya Hospitali ya St.George ili kulipia nauli ya usafiri wake kwenye majaribio. Alifunga ndoa na Tiffany Gabriella mwezi Desemba 2020. [1]

Marejeo hariri

  1. Gleeson, Mark (14 August 2019). "New Chippa star Maphangule breaks the hearts of Sundowns with last minute equaliser". SowetanLIVE. Iliwekwa mnamo 21 March 2021.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gregory Damons kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.