Hamida Mohamedi Abdallah

Hamida Mohamedi Abdallah (amezaliwa tarehe 28 Juni 1966) ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa Chama cha kisiasa cha Chama Cha Mapinduzi (CCM). Amechaguliwa kuwa mbunge wa Viti Maalumu kwa miaka 20152020. [1] Mwaka 2020 alirudi bungeni kama mbunge wa Lindi Mjini.

Aliwahi kufanya kazi kama mtumishi wa Umoja wa Wanawake wa CCM na katika halmashauri ya Lindi kabla ya kuingia bungeni.[2]

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania Ilihifadhiwa 25 Januari 2020 kwenye Wayback Machine., iliangaliwa Mei 2017
  2. Hon. Hamida Mohamedi Abdallah, tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Aprili 2022