Happiness Magese (pia anajulikana na jina la Millen Magese) ni mwanamitindo na mfanyabiashara wa Tanzania. Alikuwa mshindi wa mashindano ya Miss Tanzania mwaka 2001.[1]

Aliiwakilisha nchi yake katika mashindano ya urembo ya Kimataifa Miss World 2001, yaliyofanyika nchini Afrika Kusini. Alipata fursa hiyo akiwa na umri wa miaka 22.

Baada ya kushiriki katika mashindano hayo, alirejea nchini kwake akasafiri tena nchini Afrika Kusini kuwa mwanamitindo. Alipata umaarufu sana katika kazi yake na sasa anajulikana kama mwanamitindo wa kimataifa.

Tanbihi hariri

  1. "Former Miss Tanzania Millen Magese: Endo Sent Me To The Hospital 'Every Month'". Endometriosis : Causes - Symptoms - Diagnosis - and Treatment (kwa Kiingereza). 2018-04-11. Iliwekwa mnamo 2024-04-04. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Happiness Magese kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.