Hawa Abdi
Hawa Abdi Dhiblawe[1] (Somali: Xaawo Cabdi, Arabic: حواء عبدي, alizaliwa tarehe 17 Mei 1947 na kufariki tarehe 5 Agosti 2020) alikuwa mwanaharakati wa haki za binadamu na daktari kutoka Somalia. Alikuwa mwanzilishi na mwenyekiti wa Taasisi ya Dr. Hawa Abdi (DHAF), ambayo ni shirika lisilo la faida.
Hawa Abdi alizaliwa mjini Mogadishu na aliishi katika eneo la kusini-mashariki mwa Somalia. Mama yake alifariki alipokuwa na umri wa miaka 12. Baada ya hapo, Abdi alichukua jukumu la kazi za nyumbani, ikiwemo kulea dada zake wanne wadogo.[2] Baba yake alikuwa mtaalamu na alifanya kazi katika bandari ya jiji kuu.
- ↑ "Dr. Hawa Abdi, M.D.: Physician & Human Rights Activist, Hawa Abdi Foundation". In-Sight Publishing (kwa Kiingereza). 2013-08-18. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
- ↑ "Dr. Hawa – Dr. Hawa Abdi Foundation". web.archive.org. 2017-03-02. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-02. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.