Hezi

(Elekezwa kutoka Hertz)

Hezi, pia hertz , kifupi Hz ni kipimo cha SI kwa marudio ikitaja rudio 1 kwa sekunde 1. Inatumiwa hasa kwa kutaja tabia ya mawimbi kama wimbisauti au mawimbi sumakuumeme za redio na pia marudio katika mitambo kwa mfano kompyuta.

Kipimo hiki kilipokea jina lake mwaka 1930 kwa heshima ya mwanafizikia Mjerumani Heinrich Hertz aliyekuwa mtaalamu wa kwanza wa kuonyesha kuwepo kwa mawimbi sumakuumeme.

Ngazi za Hz

hariri

Kipimo cha Hz hutumiwa mara nyingi kwenye ngazi zifuatazo:

Jina Kifupi Zaomtiririko Marudio/sekunde Mifano
Kilohezi (Kilohertz) kHz     Marudio 1000 kila sekunde. Sauti za juu sana katika muziki zina kHz kadhaa hadi 20 kHz.
Megahezi (Megahertz) MHz     marudio milioni 1 kila sekunde. Vituo vya redio vya FM hutumia mawimbi ya sumakuumeme yenye marudio mnamo 100 MHz.
Gigahezi (Gigahertz) GHz     marudio bilioni 1 kila sekunde. CPU za kompyuta huwa na marudio katika kiwango cha GHz kadhaa.
Terahezi (Terahertz) THz     marudio triliardi 1 kila nukta. Nuru huwa na marudio kwenye kiwango cha 1000 THz.
Petahezi (Petahertz) PHz     Mnururisho wa Eksirei unafikia hapa.
 
Mfano wa mwanga unaowaka kwa marudio ya a)  , b)  na c)  . f ni alama ya Hz katika fomula; 1 Hz inamaanisha ya kwamba taa inawaka maa 1 kila sekunde. 0.5 Hz inamaanisha inawaka nusu kila sekunde = mara 1 kila sekunde 2; 2 Hz inawaka mara 2 kila sekunde. T ni alama ya wakati katika fomula, inataja kipindi cha marudio yaani ni seknde ngapi kutoka kuwaka hadi kuwaka.

Matumizi

hariri

Sauti ni wavu inayosambaa kwa mbembeo wa shinikizo. Masikio ya kibinadamu husikia marudio ya sauti katika upeo wa sikio kama sauti za juu au sauti za chini. Kila noti ya muziki inalingana na marudio fulani yanayopimika kwa hertz. Sikio la mtoto mchanga husikia sauti kuanzia hezi 20 hadi hezi 20,000. Kwa mtu mzima uwezo wa kusikia sauti za juu hupungua kwa sababu ngozi ya kiwambo cha sikio kupoteza ulaini wake na mtu mzima kwa kawaida husikia marudio hadi 16,000 Hz pekee.

Sauti juumno ni sauti juu ya 20,000 Hz hadi upeo wa MHz na kipimo hiki hutumiwa kupima mitetemo ya molekuli.

Mnururisho sumakuumeme

hariri

Mnururisho sumakuumeme hupatikana kama mawimbi ya redio, eksirei, nuru na joto. Tofauti kati ya aina hizi huelezwa kwa idadi ya marudio yake kwa sekunde au kipimo chake kwa Hz. Mawimbi ya sumakuumeme hupita kila mahali bila kutegemea midia ambayo ni tofauti na wimbisauti. Yanapita hata katika ombwe.

  • Wimbi redio kwa kawaida hupimwa kwa kilohezi (kHz), megahezi (MHz) au gigahezi (GHz).
  • Mwanga ni mnururisho sumakuumeme pia lakini marudio yake ni ya juu zaidi. Upo katika upeo wa terahezi makumi (nuru ya infraredi) hadi maelfu (urujuani mno).
  • Mnururisho wa gamma hupimwa kwa exahezi yaani 1018 Hz huu ni kipimo cha marudio ya unurunifu.

Kompyuta

hariri

Uwezo wa kompyuta na hasa CPU yake hupimwa pia kwa kutaja marudio ya CPU kwa kipimo cha Hz.

Kompyuta za kwanza zilikuwa na marudio wa 4 Hz. Kompyuta ya binafsi aina ya PC ya kwanza iliyouzwa nakampuni ya IBM ilifikia marudio ya 4.77 MHz. Chipu ya P5 ya Intel ilifikia 100 MHz mwaka 1995. Tangu mwaka 2000 chipu za 1 GHz na zaidi zimepatikana. Maendeleo yalifikia zaidi ya 8 GHz tangu mwaka 2011.