Hezbollah
Hezbollah (kwa Kiarabu: حزب الله , ikimaanisha Chama cha Allah (Mungu) ni chama cha Waislamu wa dhehebu la Shi'a nchini Lebanoni. Chama hicho kina tawi la masuala ya kiraia na pia tawi la kijeshi.
Historia
haririChama hicho kilianzishwa tarehe 16 Februari 1985 na Sheikh Ibrahim al-Amin. Kuanzishwa huku rasmi kulifuatia kutangazwa kwa manifesto ya Hezbollah. Moja ya matamko ndani ya manifesto hiyo ni tamko la vita dhidi ya Israeli kwa kuivamia na kuikalia nchi ya Lebanoni.
Kutokana na uvamizi huo, Hezbollah iliingia katika kipindi cha mapambano na Israeli hadi mwaka 2000 ambapo Israeli iliondoka katika maeneo iliyokuwa imeyakalia upande wa kusini mwa Lebanoni.
Hezbollah imekuwa ikiongozwa na Katibu wake mkuu, Sayyed Hassan Nasrallah hadi alipouwawa kwa shambulio la anga la Israeli mnamo Septemba 2024. Kikapita kipindi kifupi cha mpito ndipo uongozi ukachukuliwa na Ayatollah Naim Qassem tarehe 29 Oktoba, 2024.
Viungo vya nje
hariri- Tovuti ya Hezbollah Ilihifadhiwa 19 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- Luninga ya Hezbollah: Al-Manar TV Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Redio ya Hezbollah: Al-Nour radio Ilihifadhiwa 30 Januari 2009 kwenye Wayback Machine.
- Hezbollah ni akina nani?
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |