Hi5 (Tovuti)
Hi5 ni tovuti ya mitandao ya kijamii. Kampuni ilianzishwa mwaka wa 2003 na Ramu Yalamanchi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa sasa. [2] Kwanzia Januari 2009, Hi5 inadai kuwa na zaidi ya wafuasi milioni 60. [3]
Alexa rank | 51[1] |
---|
Vipengele
haririKatika Hi5, watumiaji huunda kurasa zao ili kuonyesha habari kama vile maslahi, umri na mji wa nyumbani na pia picha ya mtumiaji ambapo watumiaji wengine wanaweza kuandikachochote wanafikiria. Hi5 pia inaruhusu mtumiaji kuunda albamu binafsi ya picha na kuanzisha chombo cha kuchezea muziki katika ukurasa wake. Watumiaji wanaweza pia kutuma maombi ya rafiki kutumia Barua pepe kwa watumiaji wengine. Wakati mtu anapata ombi urafiki, anaweza kukubali au kukataa, au kuzuia mtumiaji kabisa. Wakati mtumiaji anakubali ombi la urafiki kutoka mtumiaji mwingine, wao wawili wataunganishwa mara hiyo au katika shahada ya 1. Mtumiaji huyo ataweza kuwa katika orodha ya marafiki ya mtumiaji huyu mwingine.
Baadhi ya watumiaji hupendelea kurasa zao kutazamwa na kila mtu kwenye Hi5 . Watumiaji wengine uchagua kufanya kurasa zao kutazamwa tu na wale watu walio katika mtandao wao. Mtandao huu una marafiki wa kwanza wa mtumiaji (shahada ya Kwamza ), na marafiki wa wa marafiki wake wa kwanza (Shahada ya pili) na marafiki wa marafiki wa marafiki wake wa Kwanza (Shahada ya tatu). [4]
Hisa za Soko
haririKulingana comScore, mwaka wa 2008 Hi5 ilikuwa Tovuti ya mtandao wa kijamii ya tatu katika kutembelewa kila mwezi. [5]
Ingawa iliundiwa na makao yake makuu yako nchini Marekani, ni maarufu zaidi katika nchi nyingine, hasa katika Latin Amerika, kuchukua nafasi ya 37 katika dunia tu miongoni mwa watu ambao wana chombo cha Alexa kilichowekwa katika mitandao yao [6] lakini 84 tu katika Marekani [7]
Ukosoaji
haririUlaghai mtandaoni
haririKumekuwa na barua pepe za ulaghai zinazofanana na vialiko katika Hi5. [8] [9]
Spam
haririHi5 imekuwa ikitumia mbinu spam ili kupata watumiaji zaidi. Hutuma mwaliko katika anwani yako ya Gmail kama haukuwa makini katika usajili.
Angalia pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "hi5.com - Traffic Details from Alexa". Alexa Internet, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-04-24. Iliwekwa mnamo 2009-10-17.
- ↑ Young Hispanics online, Albuquerque Tribune, 27 Aprili 2007, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-29, iliwekwa mnamo 2010-01-03
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Social-networking sites going global, USA Today, 10 Februari 2008
- ↑ Allwood, Brandon (3 Mei 2005). Entertain yourself online. Jamaica Observer. Archived from the original on 2005-05-07.
- ↑ Social Networking Explodes Worldwide as Sites Increase their Focus on Cultural Relevance, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-04, iliwekwa mnamo 2010-01-03
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-21. Iliwekwa mnamo 2022-01-07.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-16. Iliwekwa mnamo 2021-12-26.
- ↑ Hi5 "Add Friend" Malicious Spam, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-11-21, iliwekwa mnamo 2009-01-04
{{citation}}
: Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Great, One More Friend Or So You Think., Sophos, iliwekwa mnamo 2009-01-04
Viungo vya nje
hariri- hi5 - Tovuti Rasmi
- Trafiki Stats Ilihifadhiwa 7 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine. - Maelezo kuhusu Tovuti 20