Hifadhi ya Taifa ya Nairobi

Hifadhi ya Taifa ya Nairobi ilikuwa mbuga ya kwanza nchini Kenya ilipoanzishwa mwaka wa 1946. Iko takriban kilomita 7 kusini mwa katikati ya Nairobi, mji mkuu wa Kenya, na ni ndogo ikilinganishwa na mbuga nyingine za wanyama barani Afrika. Majumba marefu jijini Nairobi yaweza kuonekana kutoka kwenye mbuga.

Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi, Kenya

Mbuga hii ina wanyamapori wengi tofauti.[1] Ni ugo tu unaotenganisha mbuga hii ya wanyama kutoka mji mkuu.[2] Wanyama walao mimea hujaa sana katika mbuga hii wakati wa kiangazi. Ni mojawapo kati ya makimbilio ya vifaru yaliyofanikiwa sana nchini Kenya.

Kwamba mbuga hii ipo karibu na jiji la Nairobi husababisha mgogoro baina ya wanyama na wananchi na pia hutishia uhamaji wa wanyama.

Tanbihi

hariri
  1. Riley 2005, p.90
  2. Prins 2000, p.143