Kilomita (pia: kilometa) ni kipimo cha urefu. Kinamaanisha urefu wa mita 1,000. Kifupi chake ni km.

Ufafanuzi wa awali wa kilomita

Kilomita ni kipimo cha kawaida katika maisha ya kila siku cha kupimia umbali usio karibu. Umbali kati ya miji hupimwa kwa kilomita.

Kilomita ni sehemu ya vipimo vya SI vyenye msingi wa mita.

Katika nchi mbalimbali kilomita imechukua nafasi ya vipimo vingine kama maili au verst.

Kwa umbali mkubwa mno kama kwa vipimo vya astronomia kilomita haifai tena. Hapo kuna vipimo vingine. Kwa mfano umbali kati ya mwezi na dunia inaweza kutajwa kwa kilomita ni lakhi tatu au km 300,000. Umbali kati ya Dunia na Jua ni km 150,000,000 na kwa umbali huo kizio cha kizio astronomia hutumiwa. Lakini umbali kutoka jua letu hadi nyota nyingine ni mkubwa mno. Hapa vipimo kama mwakanuru au pia parsek hutumiwa.