Hifadhi ya Taifa ya Pongara
Hifadhi ya Taifa ya Pongara ni mbuga ya taifa nchini Gabon karibu na mji mkuu wa Libreville, upande wa kusini wa Gabon na Bahari ya Atlantiki . Ina eneo la kilomita za mraba 929. Hifadhi hiyo inaundwa hasa na misitu yenye unyevunyevu ya kitropiki na misitu ya mikoko .
Maelezo
haririHifadhi ya taifa ya Pongara iko upande wa kusini wa Gabon na ina eneo la ukubwa wa hektari 96,302. Mahali hapo pana misitu na ina anuwai ya makazi ikiwa ni pamoja na msitu wa mikoko, msitu wa kinamasi, msitu wa mito na msitu uliofurika kwa msimu. Pia kuna ukanda mrefu wa eneo la ufuo wa mchanga na savanna yenye nyasi. Mito kadhaa hutiririka kupitia kwenye hifadhi hiyo hadi kwenye mwalo wa maji, ikiwa ni pamoja na Mto Remboué, Mto Igombiné na Mto Gomgoué.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Pongara kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |