Savana
Savana ni aina ya sura ya nchi yenye manyasi na kiasi kidogo cha miti ambacho kinategemea kiasi cha maji au mvua kinachopatikana.
Tabia kuu ya savana ni uhaba wa maji. Tofauti na jangwa maji yapo ingawa kidogo. Kiwango cha kawaida cha mvua ni kati ya milimita 500 na 1500 kwa mwaka.
Savana ina wanyama wa pekee wanaomudu mazingira hayo. Wengi ni wala majani halafu kuna wala nyama wanaowinda wala majani.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|