Historia ya Mpira wa Kikapu
Historia ya Mpira wa Kikapu ilianza baada ya kugunduliwa mnamo mwaka 1891 huko springfield, Massachusetts na mwalimu wa mazoezi ya mwili James Naismith kutoka huko kanada amabapo ilijulikana kuwa ni mchezo unaochezwa bila ya kupatikana majeraha mengi kwa wachezaji wake ukilinganisha na mpira wa miguu. Naismith alikuwa na umri wa miaka 31, aliyehitimu masomo yake, pindi alipogundua mchezo huu wa ndani ili kujiweka sawa na michezo ya majira ya baridi. Mchezo huu ulikuwa sana na kujulikana na watu wengi katika karne ya 20 na kuendelea, mara ya kwanza nchini marekani na hadi sehemu mbalimbali za dunia.
Baada ya Mpira wa Kikapu kuanza kuchezwa sana katika vyuo vya kati huko marekani ndipo ulipoanza kuchezwa rasmi katika maeneo tofauti tofauti nchini humo. Taasisi ya mpira wa kikapu ijulikanayo kama National Basketball Association (NBA), ilianzishwa mnamo mwaka 1946, na kuwa taasisi kubwa sana na inayo ingiza mabilioni ya pesa na kuajiri watu wengi kipindi cha mwishoni mwa karne hio. Na hivyo Mpira wa Kikapu kuanza kuchezwa na watu wengi nchini marekani na kuwa sehemu kubwa ya maisha ya watu nchini humo.