Kanada
Kanada ni nchi kubwa ya Amerika ya Kaskazini na ya pili duniani kwa eneo baada ya Urusi, lakini idadi ya wakazi ni 39,858,480 tu (2023).
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Kilatini: A Mari Usque Ad Mare ("Bahari hadi bahari") | |||||
Wimbo wa taifa: "O Canada" Wimbo wa kifalme: "God Save the King" | |||||
Mji mkuu | Ottawa | ||||
Mji mkubwa nchini | Toronto | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza, Kifaransa | ||||
Serikali | Ufalme wa kikatiba, shirikisho, demokrasia Charles III Mary Simon Justin Trudeau | ||||
Uhuru Sheria ya 1867 Mkataba wa Westminster Sheria kuhusu Kanada |
1 Julai 1867 11 Desemba 1931 17 Aprili 1982 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
9,984,670 km² (ya 2) 11.76 | ||||
Idadi ya watu - 2023 kadirio - 2021 sensa - Msongamano wa watu |
39,858,480 (ya 37) 36,991,981 4.2/km² (ya 236) | ||||
Fedha | Dollar ya Kanada ($) ( )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-3.5 to -8) (UTC-2.5 to -7) | ||||
Intaneti TLD | .ca | ||||
Kodi ya simu | +1
|
Kwenye nchi kavu imepakana na Marekani bara na jimbo la Alaska. Mbele ya pwani zake kuna kisiwa kikubwa cha Greenland ambacho ni chini ya Denmark halafu visiwa vidogo vya St. Pierre na Miquelon (Ufaransa).
Jiografia
haririKanada ni nchi kubwa ya pili duniani lakini maeneo mengi ni baridi mno, hawana watu.
Pwani ya Kanada ni ndefu kushinda nchi zote za dunia, ikipakana na Atlantiki, Pasifiki na Bahari ya Aktika.
Jumla ya wakazi milioni 40 huishi katika majimbo 10 na maeneo matatu ya kitaifa.
Katika eno la km² 9,984,670, km² 9,093,507 ni nchi kavu na km² 891,163 ni maji.
Umbali kutoka Rasi Columbia kwenye kisiwa cha Ellesmere katika kaskazini hadi kisiwa cha Middle Island katika ziwa la Erie jimboni Ontaria ni km 4,634.
Umbali kutoka Rasi Spear katika Newfoundland upande wa mashariki hadi mpaka na Alaska upande wa magharibi ni km 5,514.
Mto mkubwa kabisa nchini Kanada ni Mto Mackenzie upande wa magharibi wa nchi.
Milima
haririBaadhi ya milima mirefu zaidi ni:
- Mlima Logan (m 5,959) - Yukon kilele cha juu cha Kanada
- Mlima Saint Elias (m 5,489) - Yukon
- Mlima Lucania (m 5,226) - Yukon
- King Peak (m 5,173) - Yukon
- Mlima Wood (m 4,850) - Yukon
- Mlima Vancouver (m 4,813) - Yukon
- Mlima Fairweather (m 4,671) - kilele cha juu cha British Columbia
- Mlima Hubbard (m 4,557) - Yukon
- Mlima Walsh (m 4,507) - Yukon
- Mlima Augusta (m 4,289) - Yukon
- Mlima Strickland (m 4,240) - Yukon
- Mlima Cook (m 4,196) - Yukon
- Mlima Waddington (m 4,019) - British Columbia
- Mlima Robson (m 3,959) - British Columbia
- Mlima Queen Mary (m 3,928) - Yukon
- Mlima Columbia (m 3,741) - kilele cha juu cha Alberta / British Columbia
- Mlima King George (m 3,741) - Yukon
- Northern Twin (m 3,731) - Alberta
- Mlima Clemenceau (m 3,664) - British Columbia
- Mlima Forbes (m 3,617) - Alberta
- Mlima Assiniboine (m 3,616) - Alberta / British Columbia
- Mlima Goodsir (m 3,567) - British Columbia
- Mlima Rouanez (m 3,555) - British Columbia
- Mlima Temple (m 3,540) - Alberta
- Mlima Upton (m 3,520) - Yukon
- Mlima Sir Sandford (m 3,519) - British Columbia
- Mlima Sir Wilfrid Laurier (m 3,516) - British Columbia
- Mlima Lyell (m 3,498) - mpaka wa Alberta na British Columbia
- Mlima Farnham (m 3,493) - British Columbia
- Mlima Athabasca (m 3,491) - Alberta
- Mlima Brazeau (m 3,470) - Alberta
- Mlima Joffre (m 3,433) - Alberta / British Columbia
- Tsar Mountain (m 3,417) - British Columbia
- Mlima Mfalme George (m 3,413) - British Columbia
- Howser Spire (m 3,412) - British Columbia
- Mlima Sir Douglas (m 3,411) - Alberta / British Columbia
- Whitehorn Mountain (m 3,399) - British Columbia
- Mlima Hector (m 3,394) - Alberta
- Mlima Dawson (m 3,377) - British Columbia
- Mlima Willingdon (m 3,373) - Alberta
- Mlima Edith Cavell (m 3,363) - Alberta
- Mlima Cline (m 3,361) - Alberta
- Mlima Fryatt (m 3,361) - Alberta
- Mlima Harrison (m 3,360) - British Columbia
- Mlima Saskatchewan (m 3,342) - Alberta
- Mlima Chown (m 3,316) - Alberta
- Mlima Mike (m 3,313) - British Columbia
- Mlima Saint Bride (m 3,312) - Alberta
- Mlima Stewart (m 3,312) - Alberta
- Mlima Queen Bess (m 3,298) - British Columbia
- Mlima Ball (m 3,294) - Alberta / British Columbia
- Mlima Sir Alexander (m 3,275) - British Columbia
- Mlima Monashee (m 3,274) - British Columbia
- Mlima Good Hope (m 3,242) - British Columbia
- Iconoclast Mountain (m 3,236) - British Columbia
- Mlima Rae (m 3,225) - Alberta
- Mlima Rogers (m 3,208) - British Columbia
- Mlima Ida (m 3,200) - British Columbia
- Mlima Galatea (m 3,185) - Alberta
- Mlima Razorback (m 3,183) - British Columbia
- Mlima Monmouth (m 3,182) - British Columbia
- Mlima Findlay (m 3,181) - British Columbia
- Mlima Ethelbert (m 3,176) - British Columbia
- Mlima Aylmer (m 3,162) - Alberta
- Mlima Seattle (m 3,150) - Yukon
- Mlima Nasser (m 3,138) - British Columbia
- Mlima Raleigh (m 3,132) - British Columbia
- Mlima Grenville (m 3,126) - British Columbia
- Mlima Old Goat (m 3,120) - Alberta
- Mlima Evan-Thomas (m 3,098) - Alberta
- Mlima Cooper (m 3,094) - British Columbia
- Mlima Moloch (m 3,094) - British Columbia
- Mlima Ratz (m 3,090) - British Columbia
- Majestic Mountain (m 3,086) - Alberta
- Mlima Tatlow (m 3,063) - British Columbia
- Taseko Mountain (m 3,063) - British Columbia
- Kates Needle (m 3,053) - Alberta / British Columbia
- Mlima Templeman (m 3,050) - British Columbia
- Mlima Moore (m 3,044) - British Columbia
- Mlima Quanstrom (m 3,038) - British Columbia
- Talchako Mountain (m 3,037) - British Columbia
- Mlima Washburn (m 3,033) - British Columbia
- Mlima Ulysses (m 3,024) - British Columbia
- Mlima Tisiphone (m 3,021) - British Columbia
- The Rajah (m 3,018) - Alberta
- Mlima Vishnu (m 3,008) - British Columbia
- Mlima Hornickel (m 3,002) - British Columbia
Mingine chini ya m 3,000 ni:
- Mlima Meager (m 2,680) - British Columbia, volkeno
- Mlima Garibaldi (m 2,675) - British Columbia, volkeno
- Mlima Cayley (m 2,385) - British Columbia, volkeno
- Mlima Blackcomb (m 2,284) - British Columbia
- Golden Hinde (m 2,195) - British Columbia kilele cha juu cha kisiwa Vancouver
- Whistler Mountain (m 2,182) - British Columbia
- Bishop's Mitre - Milima Kaumajet
- Mlima Marble - Long Range
- Mlima Caubvik (m 1,652) - Milima Torngat
- Mlima Man O'War (m 1,050) - Milima Kiglapait
- Mlima Thor (m 1,675)
Historia
haririMaeneo ya Kanada yalianza kukaliwa walau 14,000 iliyopita na wahamiaji kutoka Asia ya Kaskazini.
Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa Wanorwei kutoka Greenland mnamo mwaka 1000 BK. Lakini hawakukaa muda mrefu sana.
Katika karne zilizofuata kuna uwezekano wa kwamba wavuvi kutoka Ulaya ya Kaskazini walifika pwani za Kanada mara kwa mara na kujenga makazi ya muda wakikausha samaki kwa ajili ya safari za kurudi, lakini hakuna uhakika.
Tarehe 26 Aprili 1497 alifika Mwitalia Giovanni Caboto (kwa Kiingereza huitwa "John Cabot") kwenye visiwa vya Newfoundland akiwa katika utumishi wa malkia wa Uingereza akavitangaza kuwa eneo la Waingereza.
Mnamo 1534/1535 Wafaransa walifika katika eneo la Mto Saint Lawrence na kujenga makao yao.
Wapelelezi na walowezi kutoka Ulaya walileta pamoja nao magonjwa ambayo hayakujulikana kwa wenyeji asilia na yalisababisha vifo vingi kati yao. Kupunguzwa kwa wakazi asilia kulisaidia upanuzi wa walowezi Wazungu kota Amerika.
Makoloni ya Waingereza na Wafaransa yalikua polepole. Katika Vita ya Miaka Saba Ufaransa ulipotea maeneo yake yote yaliyotwaliwa na Uingereza. Visiwa vya St. Pierre na Miquelon pekee vilibaki upande wa Ufaransa. Uingereza uliamua kukubali utamaduni wa pekee wa wakazi Wafaransa katika jimbo la Quebec. Hadi leo wanaendelea kutumia Kifaransa na kufuata hasa Ukatoliki, tofauti na Wakanada wenye asili ya Kiingereza walio zaidi Waprotestanti.
Wakati wa vita ya kupigania uhuru wa Marekani, wakazi wa Kanada walibaki upande wa Uingereza. Hivyo Kanada iliendelea chini ya Uingereza ikaitwa "Amerika ya Kaskazini ya Kiingereza".
Mwaka 1841 sehemu mbalimbali ziliunganishwa kama koloni moja la Kanada.
Mwaka 1867 Bunge la Uingereza lilikubali sheria iliyounda Shirikisho la Kanada lenya majimbo manne ya Ontario, Quebec, Nova Scotia na New Brunswick. Sasa Kanada ilikuwa nchi ya kujitawala chini ya Mfalme wa Uingereza.
Kujengwa kwa reli kati ya Atlantiki na Pasiki na kufika kwa wahamiaji kutoka Ulaya kuliimarisha nchi mpya. Majimbo mapya yaliundwa hadi kufika majimbo 10 na maeneo matatu chini ya shirikisho jinsi ilivyo sasa.
Kanada ilishikamana na Uingereza katika vita kuu za dunia zote mbili. Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia nchi ilionekana kama nchi ya pekee iliyotoa sahihi yake yenyewe pamoja na Uingereza chini ya mkataba wa Versailles.
Mwaka 1927 ilipeleka balozi wa kwanza huko Marekani.
Uhuru kamili ulipatikana mwaka 1982. Hadi leo malkia wa Uingereza ni mkuu wa dola akiwakilishwa na gavana mkuu.
Miji
haririZaidi ya nusu ya wakazi huishi katika miji mikubwa zaidi. Mji mkubwa ni Toronto yenye wakazi milioni 5.6 ambayo ni bandari kwenye Ziwa Ontario na kitovu cha viwanda. Montreal ni mji wa biashara wenye milioni 3.27.
Miji mingine mikubwa ni (idadi ya wakazi katika mabano):
Majimbo
hariri- Alberta - AB
- British Columbia - BC
- Manitoba - MB
- New Brunswick - (Kiingereza) NB (Kifaransa) NB
- Newfoundland and Labrador - NL
- Northwest Territories - NT
- Nova Scotia - NS
- Nunavut - NU
- Ontario - (Kiingereza) ON (Kifaransa) ON
- Prince Edward Island - PE
- Quebec - (Kifaransa) PQ
- Saskatchewan - SK
- Yukon - YU
Watu na lugha
haririWakazi asilia wa Kanada ni Waindio na Waeskimo walioingia Amerika kutoka Siberia (Asia). Hakuna hakika walikuwa wangapi wakati wa kufika kwa Wazungu lakini idadi yao ilipungua haraka kwa sababu watu kutoka Ulaya walileta magonjwa ya kuambukizwa na wenyeji walikosa kingamwili dhidi yake. Leo hii idadi imeongezeka tena kiasi: kuna takriban milioni 1.4 au asilimia 4.9 za Wakanada wote.
Wahamiaji kutoka Ùfaransa walitangulia, wakifuatwa na Waingereza, Waskoti na Waeire. Wengine walifuata kutoka Ujerumani, Italia, Urusi, Ukraine, Poland na penginepo. Kwa jumla wenye asili ya Ulaya ni 69.8%.
Katika miaka ya nyuma wahamiaji wengi wamefika kutoka China na Asia. Wahindi wengi waliofukuzwa Uganda wamehamia Kanada pia. Kwa sasa wenye asili ya Asia ni 19.3%, wakati wenye asili ya Afrika ni 3.8%. Wakazi asili ni 6.1%
Lugha rasmi ni Kiingereza (lugha mama ya 54%) na Kifaransa (19%). Lakini zinatambulika pia lugha 9 za kijimbo.
Upande wa dini, kadiri ya sensa ya mwaka 2021, kati ya wakazi 53.3% ni Wakristo. Kati yao, madhehebu makubwa ni: Wakatoliki (29.9%), Kanisa la Muungano la Kanada (3.3%) na Anglikana (3.1%). Waislamu ni 4.9%, Wahindu 2.3%, Singasinga 2.1%, Wabuddha 1.0%, Wayahudi 0.9%. Kwa jumla dini zinarudi nyuma, hazithaminiwi, tena tayari 34.6% hawana dini yoyote.
Tazama pia
haririViungo vya nje
hariri- Taarifa za jumla
- Canada Ilihifadhiwa 4 Februari 2009 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Kanada katika Open Directory Project
- Canada from BBC News
- Canada Ilihifadhiwa 30 Aprili 2019 kwenye Wayback Machine. from CIA World Factbook
- Canada profile from the OECD
- Canadiana: The National Bibliography of Canada from Library and Archives Canada
- Key Development Forecasts for Canada from International Futures
- Serikali
- Official website of the Government of Canada
- Official website of the Governor General of Canada
- Official website of the Prime Ministers of Canada
- Utalii
- Canada's official website for travel and tourism
- Official website of Destination Canada Ilihifadhiwa 26 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine.
- Masomo
- A Guide to the Sources Ilihifadhiwa 22 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine. from International Council for Canadian Studies
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|