Hospitali ya Karatu

Hospitali ya Karatu ni hospitali inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania katika Dayosisi ya Kaskazini.

hospitali ya kanisa la Kilutheri la Karatu

Ilianzishwa mwaka 2002 na Frank Artress akishirikiana na Susan Gustafson walipopata changamoto ya ukosefu wa huduma za Afya walipotembelea nchini Tanzania kwa shughuli za Utalii.

Hospitali ina vitanda 90 ila havitumiki vyote. Hospitali ina madaktari 3, maafisa wa kliniki 4, manesi 24 na wafanyakazi wengine 47. Jumla ya wafanyakazi wote ni 78. Inasimamia zahanati 6 na Kliniki 1.[1]

Marejeo

hariri