Daktari
Daktari (au dokta; wingi wake unaundwa kwa kutanguliza ma-) ni neno lenye asili ya Kilatini ("doctor") lililoingia Kiswahili kwa kupitia Kiingereza. Hutumiwa kwa maana mbili:
1) Mtaalamu aliyepata mafunzo maalum kwenye chuo kikuu cha kutibu maradhi ya wagonjwa. Mtu wenye ujuzi wa kutibu anaitwa pia mganga (wa), tabibu (ma). Daktari humtibu mgonjwa kwa kutumia sindano, kumtundikia dripu n.k. baada ya kumpima baadhi ya vitu kama:
- Kumpima damu
- Kumpima mapigo ya moyo n.k. Maranyingi daktari hufanya kazi yake katika sehemu maalumu iitwayo Hospitali.
2) Kwa kufuata tabia za lugha nyingine daktari hutumiwa pia kama jina la heshima kwa mtu aliyepata shahada ya uzamivu au "PhD" ambayo ni shahada ya juu kabisa.
Picha
hariri-
Madaktari wakimtibia mgonjwa
-
Daktari wa meno
-
Madaktari wa kufanya upasuaji.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Daktari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |