Hospitali ya Mafunzo na Marejereo ya Moi
Hospitali ya Mafunzo na Marejereo ya Moi ni hospitali iliyoko katika maeneo ya mashambani ya Magharibi mwa Kenya katika jiji la Eldoret, wilaya ya Uasin Gishu, Kaskazini mwa Jimbo la Rift Valley. Iko kama kilomita 320 kaskazini Magharibi mwa Nairobi. Hospitali hii iko kando ya barabara ya Nandi, Mashariki mwa jiji la Eldoret. Kuna vielekezo kadhaa kando ya barabara vya kuwaongoza wageni na wagonjwa hadi hospitalini.
Huduma
haririHospitali hii hutoa huduma kadhaa katika vitengo vitatu vikuu vikiwemo: Uponyaji, Ukingaji na Urudishaji hadi afya.
Huduma za 'Outpatient'
haririKitengo hiki katika jumba kuu la OPD na ipo kando ya barabara. Kiungo hiki kiko na wataalam wa kazi tofauti. Hospitali imepakwa rangi tofauti kuonyesha cliniki tofauti zilizopo, zikiwemo: 'Ambulatory Clinic'(nyekundu), 'Reproductive'(Tango Red), Mtoto mgonjwa(manjano), 'Consultant Clinic'(Venetian Green) na 'Accident & Emergency(Baby Blue)' pamoja na idara nyinginezo.
Huduma za Ajali na Dharura
haririKitengo hiki kimefunguliwa masaa 24 ya siku na liko tayari kushughulikia dharura yoyote. Liko na vyumba vya dharura, operesheni ndogo, 'plaster', 'x-ray', kata ya uchunguzi na huduma za maabara.
Huduma za Meno
haririHuduma maalum ni pamoja na: kujazwa mashimo ya meno, urekebishaji wa taya zilizovunjika na kung'olewa meno.
Huduma za chumba cha operesheni cha Majaliwa
haririJumba hili lina vyumba vidogo vya operesheni na hivi ni pamoja na: Arap Samoei, Lenana, Mathews, George Rapp na Adamba.
Kitengo cha kujali shadidi
haririKitengo hiki kina vitanda tano na huhudumia wote watoto na watu wazima.
Kliniki za Ushauriano na Wataalam
haririKliniki hizi huendeshwa katika siku maalum za wiki kwa sababu ya miadi ama aitha kama rejereo kutoka kwa makliniki mengine ya hospitali hiyo ama hospitali nyengine. Kliniki hizi ni pamoja na :
- General Medicine
- General surgery
- General Pediatric
- Psychiatry
- General Obstetrics and Genecology
- Specialist Clinics
- Dermatology
- Ophthalmology
- Neuro-Surgery
- Plastic Surgery
- Cardio-thoracic
- Upasuaji wa Skio, Pua na Koo
- Urology
- Kliniki ya Ugonjwa wa Sukari
- Renal
- Pediatric Surgery
- Orthopedic
Huduma za 'In-Patient'
haririKuna jumla ya vitanda 550 vilivyogawika katika vitengo vya wataalam vilivyo katika hospitali hiyo na katika maeneo mawili ya kibinafsi yanayoitwa; 'Private Wing I' na 'Private Wing II'.
Huduma za Ukarabati
haririHospitali linatoa huduma zifuatazo za Ukarabati: Physiotherapy Occupational Therapy Orthopaedic Technology
'Radiology' na 'Imaging'
haririKuna vitengo viwili katika idara hii (Kitengo kikuu na cha x-ray za ajali na dharura) ambavyo hutoa huduma nyingi za uchunguzi wa x-ray, yote ya kawaida na ya kitaalam.
Maabara ya Matibabu
haririMaabara yao hutoa huduma nyingi ya matibabu, yote ya kawaida na ya kitaalam, wakitumia njia na vyombo vya kisasa katika sehemu sita ambazo ni pamoja na: 'Biochemistry', 'Microbiology', 'Immunology', 'Histology/Cytology', 'Parasitology', na 'Haematology'.
Kiwanda cha kupewa dawa
haririKiwanda hiki huweka na kupeana dawa katika hospitali hiyo na hufanya kazi masaa 24 kila siku. Kuna vituo siaba kama hivyo hospitalini nzima ili kuhakikisha kuwa wateja hawahangaiki wakichukua madawa yao
Huduma za Kuhifadhia maiti
haririHuduma zinazotolewa hapa ni pamoja na: uhifadhi wa maiti na huduma za baada-ya-kifo.
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Hospitali ya Mafunzo na Marejereo ya Moi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Angalia Pia
haririMarejeo
hariri- http://www.mtrh.or.ke/General_info.htm Archived 16 Mei 2010 at the Wayback Machine.
Viungo vya nje
hariri- http://www.mtrh.or.ke/General_info.htm Archived 16 Mei 2010 at the Wayback Machine.