Hulda Jane Stumpf (10 Januari 1867 – 3 Januari 1930) alikuwa mmisionari Mkristo raia wa Marekani ambaye aliuwawa nyumbani kwake karibu na Africa Inland Mission kituo cha Kijabe, koloni la Kenya, ambapo alikuwa anafanya kazi kama katibu na mtawala.[1]

Inawezekana Stumpf aliuwawa kwa sababu ya upinzani wake dhidi ya ukeketaji wa wanawake. Kabila kuu la Kenya, Wakikuyu, walichukulia ukeketaji kama ibada muhimu, na kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya makanisa ya kimisionari ya Kenya kwa sababu yalipinga ukeketaji huo. Nyakati hizi, zinajulikana kwenye historia ya Kenya kama Utata wa ukeketaji wa wanawake Kenya, 1929-32

Stumpf aliripotiwa kurekodi filamu dhidi ya ukeketaji nyumbani kwa mabinti wa Kijabe, ambapo aliwasaidia kutoroka. Baadhi ya majeraha yasiyo ya kawaida kwenye mwili wake yalidhihirisha kwa Gavana wa Kenya wa wakati huo kwamba, wauaji wake walimkeketa, kabla ama baada ya kumuua, hata hivyo mahakama ilihitimisha kwamba hakukuwa na uthibitisho kuwa aliuwawa sababu ya upinzani wake dhidi ya ukeketaji.

Maisha ya utotoni na elimu

hariri
 
Barua ya Stumpf ya tarehe 24 Oktoba 1906 kwa Africa Inland Mission.

Stumpf alizaliwa huko Big Run, Pennsilvania, wazazi wake ni J. R. Stumpf na mkewe, na alikulia huko Indiana, Pennsylvania, ni mmoja kati ya watoto wanne. Baba yake alimiliki duka kubwa lililoitwa Indiana's first, lililokuwa kwenye jengo namba 700 kwenye mtaa wa Filadelfia (700 block of Philadelphia Street). Alikuwa ni mmoja wa wazawa wa kwanza kumiliki gari, mwaka 1906 ni magari sita pekee ndio yalikuwa yamesajiliwa, na mwezi Julai 1901 alianza kulitumia gari hilo kupeleka bidhaa kwa wateja.[2]

Stumpf alisoma katika shule ya biashara, baadae shule ya muziki huko New York kwa miaka miwili. Baada ya masomo yake, alifanya kazi kama karani na mkalimani, kisha akajifunza taaluma ya kufupisha maneno shorthand katika chuo cha Indiana Business College.[3]

Mwezi Octoba 1906 aliomba nafasi kama mmisionari wa Africa Inland Mission (AIM), akijielezea kwenye barua yake kama "mwenye umri wa miaka arobaini na mtu mkarimu sana," lakini pia mwenye afya njema.[4] Aliandika kwenye barua yake ya maombi kuwa anataka kufanya kazi Afrika kwa sababu ya "hamu ya dhati", akiamini kwamba muda ni mchache, pale atakaporudi, na mahitaji katika nchi ya kigeni ni makubwa sana"[5]

Mwezi Novemba 1906 aliwaambia AIM kwamba alikuwa anajaribu kukwepa mfumo wa madhehebu "Kuna mfumo mmoja tu wa serikali ya kikanisa, kwa kadri ya uelewa wangu, na huo msingi wake ni maandiko, na ni maandiko pekee, ukiachana na mawazo wa mwanadamu juu ya namna ya kuliongoza kanisa"[6] Kuanzia mwezi Mei 1907 alisoma kwa miezi miwili katika chuo cha Moody Bible Institute huko Chikago ili kujiandaa kwa kazi zake za kimisionari. File lake la chuo lilimuelezea kama "Mtu mnyoofu, Mfanya biashara na mkarimu"[7]

Marejeo

hariri
  1. For date of birth and middle name, Marvin J. Newell, A Martyr's Grace, Moody Publishers, 2006, 103–104; for death, image of Stumpf's headstone, accessed 2 October 2013.
  2. Hulda Stumpf, former resident, said murdered", The Indiana Gazette, 7 January 1930; John F. Busovicki, Indiana County, Arcadia Publishing, 2003, 28.
  3. Newell 2006, 104.
  4. Hulda Stumpf, Letter to G.K. Sample Ilihifadhiwa 12 Oktoba 2013 kwenye Wayback Machine., 26 October 1906, courtesy of Wheaton College.
  5. Dana Lee Robert, American Women in Mission: A Social History of Their Thought and Practice, Mercer University Press, 1996, 211.
  6. Robert 1996, 212, n. 57.
  7. Newell 2006, 105.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hulda Stumpf kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.