IOS ni mfumo wa uendeshaji (operating system) unaoendesha vifaa vya Apple kama iPhone, iPad, na iPod Touch. Neno IOS linamaanisha iPhone Operating System au kwa sasa iOS Operating System. Ni jukwaa la programu linalowezesha vifaa hivyo kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa uzoefu wa matumizi ya kifaa husika kwa mtumiaji.

Mfumo huu wa uendeshaji umebuniwa na kusasishwa na kampuni ya Apple, na unajulikana kwa muundo wake wa usalama imara, na utangamano mzuri kati ya vifaa vya Apple. iOS hutumika katika mamilioni ya vifaa duniani kote na ni sehemu muhimu ya jumla ya mfumo wa ekolojia ya Apple.

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.