I Believe I Can Fly
"I Believe I Can Fly" ni wimbo uliotolewa mnamo mwaka wa 1996 na mwimbaji wa R&B R. Kelly. Wimbo ulitungwa, kutayarishwa, na kuimbwa na R. Kelly. Wimbo ulipata kuwepo kwenye filamu ya mwaka wa 1996 ya Space Jam.
“I Believe I Can Fly” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya R. Kelly kutoka katika albamu ya R. na Space Jam: Muziki Unaotokana na Filamu | |||||
Imetolewa | Novemba 26, 1996 | ||||
Muundo | CD single, cassette single | ||||
Imerekodiwa | 1996 | ||||
Aina | R&B Ballad Injili | ||||
Urefu | 5:22 (albamu na toleo la single) 4:40 (haririo la redio) | ||||
Studio | Jive | ||||
Mtunzi | R. Kelly | ||||
Mtayarishaji | R. Kelly | ||||
Mwenendo wa single za R. Kelly | |||||
|
"I Believe I Can Fly" ulikuwa nafasi ya #2 kwenye chati za Billboard Hot 100, #1 kwenye chati za R&B Singles, na namba #1 kwenye chati za UK. Wimbo pia umeonekana katika albamu ya Kelly ya 1998, R.. Wimbo ulipata kujishindia tuzo tatu za Grammys, na kupewa nafasi ya #406 kwenye orodha ya Rolling Stone ya Nyimbo Kali 500 za Muda Wote.
Wimbo umepata kurejewa tena na wasanii kama vile Yolanda Adams, Me First and the Gimme Gimmes, Ruth Brown, James Ingram, William Hung, Ronan Keating na Bianca Ryan. Yolanda Adams aliuimba wimbo huu na Gerald Levert wakiwa pamoja. Jim Carrey pia ameuimba wakati wa sehemu za mwanzo kabisa katika Fun with Dick and Jane (2005). Wote wawili, yaani, Katharine McPhee na Anwar Robinson wameuimba wimbo huu kwenye American Idol. Patti Labelle ameimba kiitikio cha wimbo katika toleo lake la live albamu la 1998, Live One Night Only ikiwa kama jazio la alama ya tuni yake kwenye "Over the Rainbow".
"I Believe I Can Fly" ulikuwa ukiimbwa na bendi ya shule kwenye filamu ya Drumline wakati wa sherehe za mahafali ya wanafunzi wa elimu ya juu ya Devon Miles (Nick Cannon).
Chati
haririChati (1996) | Nafasi iliyoshika |
---|---|
U.S. Billboard Hot 100 | 2 |
U.S. Billboard Hot R&B Singles & Tracks | 1 |
U.S. Billboard Dance Maxi Singles | 6 |
U.S. Billboard Adult Contemporary | 7 |
UK Singles Chart | 1 |
Australia ARIA Singles Chart | 24 |
Austrian Singles Chart | 2 |
Dutch Singles Chart | 1 |
Eurochart Hot 100 Singles | 1 |
French Singles Chart | 1 |
German Singles Chart | 3 |
Swedish Singles Chart | 11 |
Swiss Singles Chart | 1 |
Polish Singles Chart | 1 |
Kwenye space
haririSTS-122 kikundi kilisikia wimbo huu katika siku ya 10 ya safari ikiwa kama wito wa uamsho.[1]