Space Jam (kibwagizo)
Space Jam ni kibwagizo halisi cha albamu ya filamu ya mwaka wa 1996 yenye jina sawa na la albamu, ambayo ndani yake imechezwa na Michael Jordan na washiriki wote wa Looney Tunes. Albamu imeshirikisha kibwagizo cha filamu ambacho pia kilichopigwa na kutolewa na James Newton Howard. Kibwagizo hiki kilitolewa na studio ya Atlantic Records mnamo 12 Novemba 1996.
Space Jam | ||
---|---|---|
Soundtrack ya Wasanii tofauti | ||
Imetolewa | 12 Novemba 1996 | |
Imerekodiwa | 1996 | |
Aina | R&B, pop, hip hop | |
Urefu | 65:16 | |
Lebo | Atlantic | |
Mtayarishaji | Ken Ross, Craig Kallman, Dominique Trenier | |
Tahakiki za kitaalamu | ||
Mapokezi
haririKibwagizo hiki kimepokea tathmini nzuri na kilipata mafanikio mazuri kabisa kwenye chati za Billboard 200, kwa kushika nafasi ya #2. Kibwagizo hiki pia kilifanikiwa kuuza vizuri kabisa; ilitunukiwa kama platinamu mbili mfululizo chini chini ya miezi miwili baada ya kutolewa, mnamo mwezi wa Januari 1997. Mnamo mwaka wa 2001, kibwagizo kilitunukiwa Platinamu 6x. [1]
Orodha ya nyimbo
hariri- "Fly Like an Eagle" umeimbwa na Seal – 4:14
- "The Winner" umeimbwa na Coolio – 4:03
- "Space Jam" umeimbwa na Quad City DJ's – 5:07
- "I Believe I Can Fly" umeimbwa na R. Kelly – 5:22
- "Hit 'Em High (The Monstars' Anthem)" umeimbwa na B-Real wa Cypress Hill, Coolio, Method Man, LL Cool J na Busta Rhymes – 4:17
- "I Found My Smile Again" umeimbwa na D'Angelo – 6:15
- "For You I Will" umeimbwa na Monica – 4:56
- "Upside Down ('Round-N-'Round)" umeimbwa na Salt-N-Pepa – 4:16
- "Givin' U All That I've Got" umeimbwa na Robin S. – 4:04
- "Basketball Jones" umeimbwa na Barry White na Chris Rock – 5:40
- "I Turn To You" umeimbwa na All-4-One – 4:52
- "All of My Days" umeimbwa na Changing Faces wakimshirikisha R. Kelly na Jay-Z – 4:01
- That's the Way (I Like It)" umeimbwa na Spin Doctors wakimshirikisha Biz Markie – 3:49
- "Buggin'" umeimbwa na Bugs Bunny (Billy West), Daffy Duck (Dee Bradley Baker) na Elmer Fudd (Billy West) – 4:14
Single za albamu
haririMaelezo ya Single |
---|
"For You I Will" |
"I Believe I Can Fly" |
"Space Jam"
|
"Hit 'Em High (The Monstars' Anthem)"
|
"The Winner" |
"Fly Like an Eagle"
|
Tanbihi na marejeo
hariri- ↑ "RIAA Gold and Platinum Searchable Database". Iliwekwa mnamo 2009-01-23.