I Wanna Be Where You Are

"I Wanna Be Where You Are" ni wimbo uliotungwa na Leon Ware na Arthur "T-Boy" Ross kwa ajili ya Michael Jackson. Wimbo ulishika nafasi ya kumi na sita kwenye chati za U.S. pop single na nafasi ya pili kwenye chati za U.S. R&B single kunako mwaka 1972. Huu ni wimbo wake wa tatu kuingia moja kwa moja katika Top 40 pop ya vibao vikali vya enzi ya usanii wake wa kujitegemea katika stuidio ya Motown. Pia, hii ndiyo ulikuwa ushirikiano wake kwa mara ya kwanza kati ya Ware na Ross, mdogo wake wa kiume wa mwimbaji wa R&B, Diana Ross.

“I Wanna Be Where You Are”
“I Wanna Be Where You Are” cover
Single ya Michael Jackson
kutoka katika albamu ya Got to Be There
Imetolewa 2 Mei 1972
Muundo 7" single
Imerekodiwa Hitsville West, Los Angeles, California
Aina Soul
Urefu 3:16
Studio Motown
M1202F
Mtunzi Leon Ware
Arthur "T-Boy" Ross
Mtayarishaji Hal Davis
Mwenendo wa single za Michael Jackson
"Rockin' Robin"
(1972)
"I Wanna Be Where You Are"
(1972)
"Ain't No Sunshine"
(1972)

Huu ndiyo wimbo pekee wa Jackson ulioimbwa/kutumiwa tena sana na Marvin Gaye na Willie Hutch, Jason Weaver na The Fugees. Wimbo huu pia uliimbwa tena na Zakiya kunako miaka ya 90 na ulitayarishwa na Shedrick Guy kwenye studio ya A&M.

Marejeo hariri  Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu I Wanna Be Where You Are kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.