Ida Mntwana
Ida Mntwana alifanya kazi kama mshonaji mavazi akajishughulisha na siasa katika miaka ya 1950. [1] Baada ya Madie Hall Xuma kujiuzulu kama rais wa kitaifa wa Umoja wa Wanawake wa African National Congress (ANCWL) mwaka wa 1949, Mntwana alikuwa mbadala wake. Mntwana alikuwa mkali zaidi kuliko mtangulizi wake, akipanga wanawake katika maandamano, migomo na vitendo vingine vya uasi wa raia . [2] Pia alichaguliwa kuwa mmoja wa kamati kuu ya ANC (Africa National Congress ) [3]
Ida Fiyo Mntwana | |
Amekufa | 1960(umri 57) |
---|---|
Nchi | Afrika Kusini |
Majina mengine | Ida Mntwana |
Kazi yake | Mshonaji mavazi na Mwanasiasa |
Mnamo 1954, Mntwana alikuwa rais wa kwanza wa Shirikisho la Wanawake wa Afrika Kusini (FEDSAW). Alisaidia kuandaa Kongamano la Wananchi. [4] Siku ya pili ya kongamano hilo, polisi walivamia mkutano huo na kuzua mzozo kati ya wananchi na polisi. Ni Mntwana aliyetuliza wananchi kwa kuimba wimbo wa uhuru akiwa jukwaani ili kongamano liendelee vizuri. [5]
Marejeo
hariri- ↑ "60 Iconic Women — The people behind the 1956 Women's March to Pretoria (21–30)".
- ↑ Khaminwa, Muhonjia (2002). "Mntwana, Ida (fl. 1949–1955)". Women in World History: A Biographical Encyclopedia. Gale Research Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-21 – kutoka HighBeam Research.
- ↑ "Ida Fiyo Mntwana". South African History Online. 27 Agosti 2011. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Ida Fiyo Mntwana". South African History Online. 27 Agosti 2011. Iliwekwa mnamo 13 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Congress of the People - I was there | South African History Online". www.sahistory.org.za. 1 Septemba 2019. Iliwekwa mnamo 2020-07-14.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)