Igor Sledzevsky
Igor Vasilyevich Sledzevsky (kwa Kirusi Игорь Васильевич Следзевский; amezaliwa tarehe 17 Novemba 1940 mjini Moscow) ni mwanahistoria wa Umoja wa Kisovyeti na Urusi, mtaalamu wa historia ya kijamii ya Afrika na nadharia ya ustaarabu na dakta wa historia. Yeye ni Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistaarabu na Kikanda cha Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi, Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Kisayansi la Masuala ya Afrika la Idara ya Changamoto na Mahusiano ya Kimataifa ya Chuo cha Sayansi cha Urusi na mwanachama wa bodi ya wahariri ya jarida la Vostok (Mashariki kwa Kiswahili). Pamoja na hayo aliwahi kuandika makala kadhaa za falsafa ya historia.
Wasifu
haririAmezaliwa kwenye familia ya wanajeshi. Baba yake Vasily Aleksandrovich Sledzevsky aliyekuwa kanali wa Jeshi la Kisovyeti alipigana katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Urusi na Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mama yake ni Tatiana Vasilyevna Sledzevskaya.
Mwaka 1963 alihitimu katika Kitivo cha Historia cha Chuo Kikuu cha Moscow. Mwaka 1966 alimaliza uzamivu wa Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Umoja wa Kisovyeti. Mwaka 1967 alitetea tasnifu yake ya uzamivu Wahausa wa kisasa wa Nigeria Kaskazini kwenye Taasisi ile ile. Mwaka 1990 alitetea tasnifu yake ya udakta Miundo ya kihistoria na kijamii ya Afrika Magharibi. Changamoto za mahusiano kati ya viumbe vya kijamii vya asili na hali ya kihistoria katika Taasisi ya Mafunzo ya Mashariki ya Chuo cha Sayansi cha Umoja wa Kisovyeti.
Tangu mwaka 1967 anafanya kazi katika Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi. Miaka 1992-1998. alikuwa Mkuu wa Maabara ya Uchunguzi wa Kistaarabu ya Taasisi hiyo. Kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2008 alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kistaarabu na Kikanda cha Chuo cha Sayansi cha Urusi. Mwaka 2002 alikuwa ametunukiwa na nishani Kwa stahili mbele ya Nchi ya Uzalendo. Ameoa na ana mwana mmoja.
Viungo vya nje
hariri- Makala juu ya bw. Sledzevsky katika tovuti iitwayo "Wanaethnografia na wanaanthropolojia Warusi wa karne ya 20".