Ilhéu de Sal Rei
Ilhéu de Sal Rei ni kisiwa kisicho na makazi ya watu karibu na pwani ya Boa Vista nchini Cape Verde. Kinapatikana upande wa Kusini Magharibi umbali wa km 1 (mile 0.6) kutoka mji mkuu wa nchi. Eneo lake lina ukubwa wa ha 89 (sq mi 0.34)[1] na muinuko wa juu kutoka usawa wa bahari ni m 27 (ft 88.6).[2]
Kisiwa hicho kidogo kimeonyesha uwepo wa miamba ya chokaa na kuna fukwe za mchanga katika maeneo yaliyo chini ya hifadhi. Kisiwa chote ni kama mnara wa kihistoria wa asili.[2] Sehemu ya Ponta de Escuma ndio upande wa magharibi mwa kisiwa hicho. Pitio dhaifu kueleke kaskazini mwa kisiwa hicho hukitenganisha na kisiwa cha Boa Vista kwa takribani mita 500 hadi 600. Kwa upande wa ksuini, Ngome ya Duque de Bragança inapatikana.
Mnara wa taa wa Ponta da Escuma
haririKisiwa hicho kina mnara wa taa unaojulikana kwa jina la Ponta de Escuma, uliojengwa mnamo mwaka 1888, ukiwa na ngazi za saruji zenye urefu wa metre 5 (ft 16) na taa kileleni. Taa iliyopo kwa sasa ni mlingoti wa chuma umbo la duara lenye urefu wa metre 7.9 (ft 26) ikiwa na uwazi na karabai. Kulingana na NGA taa hiyo bado inafanya kazi, inaendeshwa kwa nguvu ya jua na hutoa mwangaza wa rangi nyekundu au mweupe mara tano kutegemeana na upande na hudumu kwa sekunde ishirini, mwanga huo huonekana kwa umbali wa maili.
Picha
hariri-
muonekano wa Jua likizama karibu na Sal Rei Islet
-
Kisiwa cha Ilhéu de Sal Rei
-
Ilheu de sal rei
-
Ilhéu de Sal Rei
-
Ramani ikionyesha muonekano wa kisiwa cha Cape Verde.
Marejeo
hariri- ↑ Resolução nº 36/2016 Archived 18 Januari 2021 at the Wayback Machine., Estratégia e Plano Nacional de Negócios das Áreas Protegidas
- ↑ 2.0 2.1 Protected areas in the island of Boa Vista Archived 19 Septemba 2020 at the Wayback Machine. - Municipality of Boa Vista, March 2013 (Kireno)
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ilhéu de Sal Rei kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |