Irina Olegovna Abramova (kwa Kirusi Ирина Олеговна Абрамова; amezaliwa 16 Septemba 1962) ni mchumi wa Urusi, mwanachama wa Uongozi wa Chuo cha Sayansi cha Urusi, mkurugenzi wa Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi, daktari wa uchumi na profesa.

Wasifu

hariri

Mwaka 1984 alihitimu kwa heshima katika Idara ya Kiarabu ya Kitivo cha Kijamii na Kiuchumi cha Taasisi ya Nchi za Asia na Afrika ya Chuo Kikuu cha Moscow.

Mwaka 1987 alitetea tasnifu ya uzamivu, ambayo mada yake ni Masuala ya kijamii na kiuchumi ya ukuzaji wa miji nchini Misri.

Miaka 1994-1997 alialikwa kuwa mhadhiri katika Vyuo Vikuu vya Tübingen, Bochum na Heidelberg nchini Ujerumani na Chuo Kikuu cha St. Gallen huko Uswisi.

Mwaka 2011 alitetea tasnifu ya udaktari ya Uwezo wa maliasili wa Afrika wa uchumi wa dunia wa karne ya 21 (Sababu za ndani za ushiriki wa mataifa ya Afrika katika mfumo mpya wa uchumi wa dunia).

Mwaka 2015 ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Afrika ya Chuo cha Sayansi cha Urusi.

Tarehe 28 Oktoba 2016 ameteuliwa mwanachama wa Idara ya Changamoto na Mahusiano ya Kimataifa ya Chuo cha Sayansi cha Urusi na mwaka 2017 aka mwanachama wa Uongozi wa Chuo hicho. Mbali na hayo yeye yupo katika Tume Kuu ya Kutathmini ya Shirikisho la Urusi.

Shughuli za kisayansi na kijamii

hariri

Bi. Abramova ni mtaalamu mkuu wa Idara ya Changamoto na Mahusiano ya Kimataifa ya Chuo cha Sayansi cha Urusi kuhusu masuala ya uchumi na idadi ya watu barani Afrika.

Miaka 2004 na 2005 alishiriki katika mikutano na semina zilizofanyika nchini Urusi na ng'amboni ndani ya fremu za Mradi wa Kimataifa wa Kukabiliana na Kuhalalishwa kwa Pesa haramu na Ufadhili wa Ugaidi kama mchambuzi wa Baraza la Ulaya.

Mwaka 2004 alihutubia kwenye Kongamano la Kimataifa la Mapambano ya Uhalifu wa Uchumi, linalofanyika mjini Cambridge huko Ufalme wa Muungano kila mwaka.

Kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2011 pamoja na wataalamu watokao Urusi na nchi nyingine alipanga na kufanya utafiti wa shambani katika nchi kadhaa za Ulaya na Afrika kuhusu masuala ya idadi ya watu na uhamiaji wa nguvukazi duniani.

Yeye ni mwanachama wa Baraza Maalum la Masuala ya Afrika la Chuo cha Sayansi cha Urusi na vile vile mshiriki wa zaidi ya mikutano na semina 80 za kimataifa, zilizofanyika nchini Urusi na ng'amboni.

Yeye yupo kwenye Bodi ya Wahariri ya Jarida la Asia na Afrika leo.

Zaidi ya hayo aliandika insha 110 za kisayansi zilizochapishwa katika Urusi na nchi nyingine, ikiwemo vitabu 8.

  • Medali ya Mchango mkubwa katika Uendeshaji wa Mkutano wa Kilele na Jukwaa la Kiuchumi Urusi-Afrika (2019)[1]
  • Nishani ya Stahili mbele ya Nchi ya Uzalendo ya ngazi ya pili (10 Septemba 2020) — kwa ajili ya mchango mkubwa katika sayansi na shughuli zenye miaka mingi na matunda mengi[2]

Vitabu

hariri
  1. Абрамова И. О., Поликанов Д. В. Интернет и Африка: параллельные реальности. М.: Институт Африки РАН, 2001. 180 с.
  2. I. Abramova, D. Magnusson et al. International experience in prevention of terrorist financing. (Международный опыт по предотвращению финансирования терроризма). Council of Europe, Moscow. 2005. PP. 1-400. (на англ. яз.).
  3. Абрамова И. О. Арабский город на рубеже тысячелетий. М.: Восточная литература, 2005. 256 с.
  4. Абрамова И. О., Фитуни Л. Л., Сапунцов А. Л. «Возникающие» и «несостоявшиеся» государства в мировой экономике и политике. М.: Институт Африки РАН, 2007. 198 с.
  5. I. Abramova, C. Stoll, К. Tkachenko. Germany in Africa: reconciling business and development. (Германия в Африке: бизнес и развитие). M.: Institute for African Studies RAS, 2009. PP. 1-192. (на англ. яз.).
  6. Абрамова И. О. Африканская миграция: опыт системного анализа. М.: Институт Африки РАН, 2009. 354 с.
  7. Leonid Fituni, Irina Abramova. Resource Potential of Africa and Russia’s National Interests in the XXI Century. (Ресурсный потенциал Африки и национальные интересы России в XXI веке). M., Institute for African Studies. RAS. 2010, PP. 1-212. (на англ. яз.)
  8. Абрамова И. О. Население Африки в новой глобальной экономике. М.: Институт Африки РАН, 2010. 496 с.

Marejeo

hariri
  1. "Награждение директора Института Африки И. О. Абрамовой медалью «за значительный вклад в организацию Саммита и Экономического форума Россия-Африка»". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-11. Iliwekwa mnamo 2023-02-11. {{cite web}}: no-break space character in |title= at position 42 (help)
  2. Указ президента Российской Федерации от 10 сентября 2020 г. № 552. Jalada kutoka ya awali juu ya 2023-02-11. Iliwekwa mnamo 2023-02-11.

Viungo vya nje

hariri