Józef Wesołowski
Józef Wesołowski (15 Julai 1948 – 27 Agosti 2015) alikuwa askofu wa Polandi katika Kanisa Katoliki. Alikuwa askofu mkuu kuanzia mwaka 2000 hadi alipoondolewa katika huduma na Vatikani mwaka 2014. Alikuwa Balozi wa Kitume kwa Jamhuri ya Dominika kuanzia Januari 2008 hadi alipoitwa kurudi nchini Agosti 2013. Mamlaka nchini Jamhuri ya Dominika walikuwa wakichunguza madai ya unyanyasaji wa watoto dhidi yake. Mnamo Juni 2015, Vatikani ilitangaza kwamba atapelekwa kwa kesi ya madai ya kuwa na picha za watoto wa kidhulumu, ambapo alikuwa akikabiliwa na kifungo cha gerezani.
Alifariki dunia tarehe 27 Agosti 2015 kutokana na shambulio la moyo kabla ya kuenda kwa kesi.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Pontificia Accademia Ecclesiastica, Ex-alunni 1950 – 1999" (kwa Kiitaliano). Pontifical Ecclesiastical Academy. Iliwekwa mnamo 12 Julai 2019.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |