Jackie Aygemang
Jackie Agyemang (jina lake la ukoo ni Appiah, alizaliwa 5 Desemba 1983) ni mwigizaji kutoka Ghana. Amewahi kuchaguliwa mara mbili kwa tuzo la mwigazaji bora wa kike katika uhusika na mwigizaji chipukuzi bora katika tuzo la Afrika Kisasa Academy Awards la mwaka 2008. [1]
Maisha ya Utotoni
haririAgyemang alizaliwa Kanada na ndiye kitinda mimba katika familia ya watoto watano. Maisha yake ya utotoni aliishi Kanada, na alihamia Ghana pamoja na wazazi wake mwaka 1993. Anatambulika zaidi kwa jina lake la ukoo la Appiah. Agyemang aliolewa mwaka 2005 na ana mwana mmoja.
Uigizaji
haririAgyemang alianza kuonekama kweneye filamu nyingi wakati alipoalikwa na Edward Seddoh Junior mwandishi wa Things We dDo For Love alipoigiza nafasi ya Enyonam Blagogee. Baadaye alishiriki kwenye mchezo wa kuigiza wa Tentacles, Games People Play na vipindi vingi vya Televisheni.
Bado Agyemang anakumba kuwa alikuwa ma hofu mara ya kwanza alipotokea kwenye maigizo, "Ilikuwa ni filamu ya kampuni ya Venus Production iliyoitwa Divine Love na alipaswa kumuigiza muhusika Kate, muhusika mkuu. Sina imani kama niliigiza vizuri. Nilisitasita lakini watu wengi hawakugundua hilo." Licha ya woga wake kama kama muigizaji wa mara wa kwanza alifaulu katika kumfurahisha kila mtu.
Agyemang anasema kuwa sehemu aliyoigiza vizuri zaidi ni katika Mummy's Daughter na kampuni ya Venus Films. Filamu inaeleza hadithi ya familia ya Bartels ambapo aliigiza nafasi kama binti wa mfalme. "Ninapenda jinsi nilivyoigiza na nilifurahishwa na muhusika niliyeigiza ". Kwa sasa Agyemang anaona filamu za nyumbani kama zilizoboreka. Ombi lake ni kuwa wengine waone mafanikio ya baadaye.
Uso wa Agyemang unaonekana kwenye mabango mengi na matangazo ya kibiashara kwenye runinga za Ghana ikiwa ni pamoja na tangazo la GSMF tangazo kuhusu kujikinga na VVU/UKIMWI, alishinda sura ya U.B kwenye tangazo ambalo ambalo aliwafanyia kwenye matangazo ya runinga na kwa sasa ndiye sura ya kampuni ya mtangazo ya kibiashara na mabango ya IPMC. "GSMF" ndilo lilikuwa tangazo lake la kibiashara kwenye runinga.
Filamu
hariri- Divine Love
- Deadly Assignment
- Golden Stool
- Mummy's Daughter
- Beyonce - The President daughter
- Tears of womanhood
- Love Doctor
- Fake Feelings
- Princess Tyra
- Run Baby Run
- Passion of the soul
- Pretty queen
- Total Love
- Mortal desire
- I Hate Women
- The Perfect Picture
- Her Excellence
- Spirit of a dancer
- The princes's bride
- the king is mine
- The heart of men
Marejeo
hariri- ↑ "Africa Movie Academy Awards' nominees take a bow in Josies". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-02-08. Iliwekwa mnamo 2009-10-23.
Viungo-wavuti
haririMakala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jackie Aygemang kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |