Jacqueline Mkindi
Jacqueline Mkindi (alizaliwa Januari? 1977)[1] ni msimamizi mbobevu wa maendeleo katika uga wa biashara ya kilimo ndani na nje ya nchi. Kadhalika ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAHA [2] na mwenyekiti wa makampuni ya kibiashara ya TAHA (TAHA FRESH Handling Ltd na GreenCert Ltd). Ni mjasiriamali aliyejikita zaidi katika kuunda na kubadilisha sekta ya kilimo cha bustani yenye thamani ya mamilioni ya dola nchini Tanzania[3].
Jacqueline anahudumu kwenye bodi za ushauri za majukwaa kadhaa ya Umma na Binafsi za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa. Kwa kutaja machache tu, yeye ni mwenyekiti wa Baraza la Kilimo la Tanzania (ACT) na anashiriki kwenye baraza kuu la Bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF). Pia anaiwakilisha Tanzania katika Kamati ya Ushauri ya Mfuko wa Pamoja wa Bidhaa yenye makao makuu yake huko The Hague, Uholanzi.
Zaidi ya hayo, ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Uongozi wa Maendeleo ya Chakula na Misitu Finlandi (FFD) - Hope, jukwaa la kukuza uwajibikaji wa hali ya hewa na maendeleo endelevu ili kupunguza hatari za mabadiliko ya hali ya hewa, ambapo anawakilisha Mashirika ya Wakulima wa Kusini Ulimwenguni.
Jacqueline ni Mkurugenzi Aliyeidhinishwa na alipewa Cheti cha Uendeshaji (CiDir) na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) mnamo Agosti, 2019. Amepata tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa kama Mwanamke wa Athari kwa kubadilisha kilimo, hasa sekta ya kilimo cha bustani nchini Tanzania [4]
Marejeo
hariri- ↑ https://africa4africawomen.org/the-horticultural-and-agribusiness-exploits-of-jacqueline-mkindi/
- ↑ https://www.linkedin.com/in/jacqueline-mkindi-613450123?originalSubdomain=tz
- ↑ https://www.rvo.nl/sites/default/files/2017/05/Tanzania%20Tuinbouwsecor%20Overzicht.pdf
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-07-08. Iliwekwa mnamo 2024-07-04.