Jahazi Modern Taarab
Jahazi Modern Taarab ni bendi ya muziki wa taarab kutoka nchini Tanzania. Bendi ilianzishwa mwishoni mwa mwaka wa 2006, jijini Dar es Salaam. Jahazi Modern Taarab, ndiyo kundi linaloongoza kwa sasa katika miondoko ya taarab kwa nchi ya Tanzania, na ndiyo kundi pekee lenye washabiki wengi kuliko.
Jahazi Modern Taarab | |
---|---|
Asili yake | Zanzibar Tanzania |
Aina ya muziki | Taarab |
Miaka ya kazi | 2006-hadi leo |
Wanachama wa sasa | |
Mzee Yusuf Khadija Yusuf Isha Ramadhani Leila Rashid |
Kundi limeweza kujipatia mafanikio makubwa kabisa katika medani ya muziki wa taarab. Mzee Yusuf, ndiyo kiongozi na mmiliki wa kundi, ambaye pia ndiyo mwanamuziki mgunduzi wa mtindo wa taarab za kisasa (yaani “modern taarab”).
Mzee aliungana na dada yake Bi. Khadija Yusuf, ambaye pia ni mwimbaji mashuhuri wa muziki wa taarab kwa nchi ya Tanzania. Wote wawili walianza kujipatia umaarufu na heshima kubwa kimataifa wakiwa na kundi walilokuwa zamani la muziki wa taarab la Zanzibar Stars Modern Taarab.
Muziki
haririAlbamu
haririNyimbo zao maarufu
haririMarejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jahazi Modern Taarab kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |