Jambo Bukoba
Jambo Bukoba ni shirika la huruma nchini Ujerumani. Lina watu 417 mwaka (2018). Tangu mwaka 2018, linatumia michezo ili kuboresha elimu, afya na fursa sawa kwa watoto na vijana nchini Tanzania.
Shughuli
haririJambo Bukoba inajihusisha na elimu,afya (kwa njia ya elimu ya umri,maambukizi ya VVU/Ukimwi na usafi) na Usawa wa kijinsia.Mfano wa shirika hilo ulianzishwa na chuo kikuu cha michezo Ujerumani na kuunganisha michezo katika mtaala wa shule kwa elimu ya uzoefu. Mkakati huo pia unakuza ushiriki wa walimu,Wazazi na maisha ya Umma na Kuboresha ujuzi wa walimu na miundombinu ya shule.Lengo ni kusaidia na kuwawezesha watoto na vijana katika mazingira yao ya kila siku ya shule ili kuwa na Mwanzo bora katika maisha na matarajio mazuri kwa ajili ya kuunda na Kuboresha siku zao wenyewe.
Mbinu
haririKutoka Ofisi ya Bukoba,Kampuni ya Tanzania inafanya miradi katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa nchi.Miradi hii inajengwa juu ya nguzo tatu: maendeleo ya walimu,mashindano ya michezo na miradi ya Ujenzi wa shule.
• Wafanyakazi wa Jambo Bukoba huandaa warsha za walimu huko Tanzania.Washiriki watajifunza katika dhana ya Jambo Bukoba na michezo maalum iliyoundwa na Chuo Kikuu cha michezo cha Ujerumani.Wataalam wa matibabu wanakuja kutoa elimu ya VVU/UKIMWI.Aidha, walimu wanatengenezwa kama vizidishi
• Mashindano ya michezo ya wazi ambayo yanajumuisha michezo ya Jambo Bukoba yanaendeshwa.Inajulikana kama Bonanza,lengo la masshindano haya si juu ya utendaji wa michezo lakini juu ya usawa wa jinsia,mchezo wa haki na kazi nzuri ya timu.Shule nne zinaishi pamoja katika kila wilaya.Mwisho wa Bonanza ya kikanda hufanyika mara moja kwa mwaka wakati wa Wanafunzi wa vyuo vikuu ambavyo wanashindana.Hii ni tukio kubwa kwa washiriki wote na roho ya furaha na sherehe ya muziki na dansi.
• Shule ambayo inashinda katika Bonanza la Mkoa inashinda fursa ya kutekeleza mradi wa Ujenzi wa shule.Shule huamua mahitaji yake ya haraka zaidi ya Ujenzi.Jambo Bukoba hutoa asilimia 75 ya gharama ya jumla ya mradi na shule hutoa asilimia 25 iliyobaki katika fomu ya fedha,muda wa kazi au vifaa.
• Katika uwanja wa mradi wa ‘’WASH’’ (Maji,Usafi na Mazingira) matanki ya maji kwa ajili ya kukusanya maji ya mvua na vifaa vya kunawia mikono ikiwa ni pamoja na sabuni vilijengwa katika shule 8.Aidha,Mafunzo ya utunzaji kwa walimu yalitolewa ili Kuboresha ujuzi kuhusu utunzaji kwa ujumla.Mnamo mwaka 2018,Vichungi 8 viliwekwa ili kuhakikisha ubora wa maji ya kunywa.
Maoni juu ya hali ya Tanzania
haririAsalimia 44.8 ya wakazi milioni 56 wa Tanzania wako chini ya umri wa miaka 15.Matatizo ya ujumla:Ushiriki wa shule sio wakawaida.Watoto wengi hujifunza shule kwa urahisi au wanaacha shule mapema.Hasa wasichana wamekuwa katika hali mbaya:mara nyingi wanapaswa kufanya kazi,kusaidia nyumbani au kukaa mbali na shule wakati wa hedhi kwa sababu ya uhusiano wake na aibu.pia wanapaswa kukabiliana na mimba za utotoni,hatari za VVU/UKIMWI hasa katika swala la ubaguzi.Asalimia 70 ya walioambukizwa VVU/UKIMWI ni kati ya umri wa miaka 15 na 20 Asilimia 75 kati yao ni wasichana. [1]Asilimia 29 ya watu wenye umri wa miaka 15 hawawezi kusoma na kuandika. Clemens Mulokozi, Mwanzilishi wa Jambo Bukoba, aliishi Tanzania kati ya umri wa miaka mitano na kumi na mbili. Miaka hiyo ilikuwa motisha yake binafsi ili kuboresha hali ya wasichana na wavulana Nnchini Tanzania.
Matokeo
hariri• Watoto 516,413 wenye umri wa kwenda shule wamefahamishwa na kusaidiwa na dhana ya Jambo Bukoba
• Shule 884 na waalimu 1,730 wamejiunga na warsha na miradi ya Ujenzi wa shule
• Miradi 57 ya Ujenzi wa shule imetekelezwa (mafano vyoo,madarasa n.k)
• Mashindano 55 ya michezo (Bonanza) yamefanyika huku zaidi ya watoto 9,000 wa shule wakishiriki katika ngazi ya wilaya na mikoa
• Ujumbe wa mara kwa mara wa vyombo vya habari wa Jambo Bukoba kupitia mtandao,televisheni,redio na magazeti
• Tasnifu 3 za uzamili/shahada
Uchapishaji wa Kitabu cha ‘’Ujuzi wa maisha kupitia michezo,Mwongozo wa Mwalimu’’ cha Sebastian Rockenfeller[2]
Mnamo mwezi Agosti mwaka 2014,Shirika la Ujasiriamali la kijamii Ashoka lilifanya utafiti wa walimu juu ya athari za Jambo Bukoba katika shule mbili zinazoshiriki katika mkoa wa Kagera.Walimu huyo walikiri kuwa
• Kiwango cha Mahudhurio kiliongezeka
• Idadi ya wanafunzi wa shule ya msingi ilikuwa bora
• Wasichana walipata kiwango cha juu cha wastani
• Wasichana walikuwa na fursa zaidi ya kushiriki katika michezo shuleni
• Ujuzi wa elimu uliimarishwa na warsha
• Elimu ya VVU na UKIMWI iliboreshwa
Shirika
haririShirika kuu la Ujerumani hufadhili shughuli kupitia ada ya uanachama na shughuli za kukusanya fedha.Pia inahusika katika mahusiano na Umma,mipango ya kimkakati,udhibiti wa bajeti na usimamizi wa uendeshaji kwa ushirikiano na timu za mradi nchini Tanzania.Wafanyakazi wa kujitolea,Wafanyakazi wa muda wote na Clemens Mulokozi wanafanya kazi ya kila siku ya Jambo Bukoba nchini Ujerumani na Tanzania.Nchini Ujerumani ,gharama za usimamizi wa ofisi hupatikana na wafuasi wa makampuni na msingi katika fomu ya mchango wa nyenzo na huduma.Hivyo asilimia 100 ya misaada ya kibinafsi inaweza kupelekwa nchini Tanzania. Jambo Bukoba ni kujitolea kwa viwango vya uwazi viliyoanzishwa na shirika la Initiative Trasnparente Zivilgesellschaft (Kazi kwa Uwazi wa Jamii ya Kiraia). [3] Jambo Bukoba ni mwanachama wa Deutsche spendenrat (Huduma ya Uhamiaji ya Ujerumani) na VENRO (Ushirikiano wa mashirika yasiyo ya maendeleo ya Ujerumani na misaada ya kibinadamu).
Waunga Mkono
haririUfuatao ni uteuzi wa makampuni ambayo yanaunga mkono Jambo Bukoba [4]
• Allianz SE
• Ashoka
• Ofisi ya Nje ya Ujerumani
• Ubalozi wa Tanzania Nchini Ujerumani
• Kampuni ya Deutsche Post DHL AG
• Chuo Kikuu cha Michezo cha Koln
• Wafanyakazi wa FC Bayern Munich
• Wizara ya Mkoa wa Kagera
• Pro 7 Sat 1 ( kituo cha Televisheni cha Ujerumani)
• Benki ya Unicredit AG (Zamani:HypoVereinsbank)
• UNOSDP
Malengo
hariri• Maendeleo ya dhana ya Jambo Bukoba katika mikoa mingine ya Tanzania kwa lengo la kuifikia nchi nzima
• Kuongezeka kwa dhana ya sasa kwa vijana wazima kama chuo kikuu katika Mkoa wa Kagera
Tuzo
haririMwaka 2015, Kansela wa jamuhuri ya shirikisho ya Ujerumani Angela Merkel alitambua Jambo Bukoba na Tuzo ya kitaifa ya Startsocial. [5] Clemens Mulokozi, mwanzilishi wa Jambo Bukoba,alichaguliwa kuwa Mshirika wa Ashoka mnamo mwaka 2016. [6]
Marejeo
hariri- ↑ Tanzania Commission for AIDS (TACAIDS) (2013) and Tanzania HIV/AIDS and Malaria Indicator Survey 2011-12. Retrieved on November 08th 2016
- ↑ „Jambo Bukoba“ – Ein Kurzzeitprojekt in Tansania zur Förderung des Schulsports. Retrieved on November 08th 2016
- ↑ Jambo Bukoba is a member of the organization "Initiative Transparente Zivilgesellschaft". Ilihifadhiwa 19 Novemba 2018 kwenye Wayback Machine. Retrieved on November 08th 2016
- ↑ 100 % of every private donation are for Tanzania! Ilihifadhiwa 22 Agosti 2017 kwenye Wayback Machine. Retrieved on August 29th 2016.
- ↑ award-ceremony for startsocial in the chancellors office of Germany. Ilihifadhiwa 12 Februari 2022 kwenye Wayback Machine. on June 17th of 2015, Retrieved on August 29th 2016.
- ↑ Videoportrait of Ashoka Fellow Clemens Mulokozi. Ilihifadhiwa 18 Agosti 2016 kwenye Wayback Machine. Retrieved on August 29th 2016.