James Cagney
James Cagney (Julai 17 1899 Machi 30 1986) alikuwa mwigizaji wa filamu kutoka Marekani. James alipata umaarufu zaidi kwa filamu za Hollywood. Alisifika sana kwa nyusika zake za kihuni na kijambazi. Alianza kazi yake ya sanaa kwenye Broadway kabla ya kuingia kwenye filamu. Umaarufu wake ulipanda haraka baada ya kuigiza katika filamu ya "The Public Enemy" mnamo 1931, ambapo alicheza kama Tom Powers, mhuni wa ghetto. Uigizaji wake katika filamu hii ulimletea sifa kubwa na kumfanya kuwa nyota.
Miongoni mwa filamu zake maarufu ni pamoja na "Angels with Dirty Faces" (1938). Humo alicheza kama Rocky Sullivan. "Yankee Doodle Dandy" (1942), alionyesha vipaji vyake vya kuimba na kucheza densi na kushinda Tuzo ya Academy kama Mwigizaji Bora. Filamu nyingine maarufu ni "White Heat" (1949), ambayo aliigiza kama Cody Jarrett, mhuni katili na mbabe.
Viungo vya Nje
hariri- James Cagney at the Internet Broadway Database
- James Cagney at the Internet Movie Database
- Kigezo:TCMDb name
- Kigezo:AllMovie name
- Kigezo:Rotten Tomatoes person
- FBI Records: The Vault - James Cagney Archived Aprili 30, 2017, at the Wayback Machine at fbi.gov
- Photographs and literature Archived Oktoba 26, 2006, at the Wayback Machine
- James Cagney in the 1900 US Census Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine, 1905 NY Census Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine, 1910 US Census Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine, 1920 US Census Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine, 1930 US Census Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine, and the Social Security Death Index Archived Aprili 19, 2012, at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu James Cagney kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |