Japheth Kimutai
Japheth Kimutai (alizaliwa Lelmokwo, kaunti ya Nandi, 20 Desemba 1978) ni mwanariadha wa mbio za kati kutoka Kenya ambaye alibobea katika mbio za mita 800.
Mwaka 1998 alishinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Kuala Lumpur kwa muda wa 1:43.82. Katika mwaka huo huo alishinda ubingwa wa Afrika mita 800 huko Dakar, Senegal. Alimaliza wa nne kwenye Kombe la Dunia la IAAF mwaka 1998.
Mwaka 1999 alishinda dhahabu kwenye Michezo ya Afrika Nzima.
Mwaka 2000 huko Sydney kwa Michezo ya Olimpiki, Japheth alishindwa kufika fainali licha ya kukimbia kwa haraka zaidi na Mkenya katika michezo hiyo.
Alikuwa ameanza kazi yake vyema mwaka 1994 aliposhinda nishani ya fedha katika Mashindano ya Dunia ya Vijana na kisha mwaka 1997 wakati bado Mdogo aliweka rekodi ya dunia ya vijana katika mbio za mita 800 kwa muda wa 1:43.64 mjini Zürich mnamo 13 Agosti 1997. Rekodi ya vijana ya dunia ilipigwa na Abubaker Kaki wa Sudan mwaka wa 2008.[1]
Kwa sasa ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Riadha cha Michezo Kamili, Kaptagat.
Marejeo
hariri- ↑ IAAF, 7 June 2008: Dibaba’s World record and Kaki’s World Junior mark leaves Oslo in awe
Makala hii kuhusu Mwanariadha wa Kenya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Japheth Kimutai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |