Jewish Week ni gazeti la kila wiki linalohudumia jamii ya Wayahudi katika jiji la New York. Jewish Week huhusisha habari, matukio, mitindo mipya na vipengele & uchambuzi wa jamii ya Wayahudi katika New York na husomwa duniani kote.

Jewish Week
Jina la gazeti Jewish Week
Aina ya gazeti *. Gazeti la kila wiki
*. Gazeti la Wayahudi
Eneo la kuchapishwa Manhattan, Long Island, Queens
The Bronx Brooklyn/Staten Island
Nchi Marekani Marekani
Mhariri Gary Rosenblatt
Mchapishaji Gary Rosenblatt
Makao Makuu ya kampuni Jiji la New York
Nakala zinazosambazwa 70,000 kila wiki
Tovuti http://www.thejewishweek.com/

Muhtasari hariri

Gazeti hili halina uhusiano wowote na shirika au muungano yoyote, lina matoleo matano ya maeneo yanayosambazwa haswa Manhattan, Long Island, Queens, The Bronx and Brooklyn/Staten Island, gazeti hufika kwa nyumbani mwa watu 70,000 kila wiki. Huu ni usambazaji wa nakala nyingi sana wa gazeti lolote la Wayahudi katika eneo la Amerika Kaskazini.

Jewish Week huhusisha makala ya Wayahudi wa New York, Marekani na Israeli pamoja na habari motomoto dunia zima ,kura za maoni, uchambuzi na maelezo. Sehemu kubwa zake ni:

• Habari za Israeli - Habari za matukio nchini Israeli kama siasa, dini na tamaduni zao.

• Habari za Wayahudi Marekani - habari kuhusu jamii ya Wayahudi kama vile sera za Marekani za ndani na za kigeni, habari za Wayahudi nchini Marekani, na kampeni za uchaguzi zinazohusu Wayahudi.

•Habari za Wayahudi wa New York - habari kutoka jamii mbalimbali katika jiji la New York na eneo linalolizunguka jiji, siasa za jiji na jimbo, maisha katika sinagogi, mashirika ya Kiyahudi na elimu ya Kiyahudi.

• Maisha ya Wayahudi - matukio ya utamaduni wa Kiyahudi na mitindo ya Kiyahudi.

• Sanaa - Vitabu vya Wayahudi,picha za sanaa , maigizo, filamu, maonyesho ya makumbusho.

• Biashara na Teknolojia - Uwekezaji wa kigeni kwa kampuni za teknolojia za Israeli.

Kuna vipengele maalum vya kila mwezi kama Fresh Ink, makala yaliyoandikwa na vijana kwa vijana, na kipengele cha kila mwaka kinachoitwa "36 Under 36" kinachohusisha vijana 36 Wayahudi wanaoathiri jamii ya Wayahudi katika jiji la New York, Israeli na nchi za kigeni.

Gary Rosenblatt ndiye amekuwa mhariri na mchapishaji tangu mwaka wa 1993.

Waandishi wa habari wanaofanya kazi katika Jewish Week ni:

  • Stewart Ain, Mwandishi wa habari wa Marekani /Israeli
  • Eric Herschthal, Mwandishi wa Sanaa
  • Randi Sherman, Mwandishi wa Chakula
  • Carolyn Slutsky, Mwandishi wa Elimu
  • Tamari Snyder, Mwandishi wa Biashara na Teknolojia
  • Sharon Udasin, Mwandishi wa Afya
  • Steve Lipman, Mwandishi wa habari wa Marekani/Israeli

Katika mwaka wa 2000, Rosenblatt na gazeti hili walishinda Medali ya Casey ya Uandishi Bora kutoka Kituo cha Uandishi cha Watoto & Familia kwa makala waliyoandika ya Stolen Innocence. Makala haya yalikuwa ripoti ya upelelezi iliyofichua miongo ya unyanyasaji wa watoto uliofanywa na mwalimu mkuu, Baruch Lanner. Makala haya yalikosolewa na wengi kuwa "uvumi". Ripoti hii ilionekana kama "njia ambayo jamii ya Orthodox hukosoa watu wanaonyanyasa watoto" na ikafanya Lanner ajiuzulu na ashitakiwe kortini.[1]

Marejeo hariri

  1. ^ http://query.nytimes.com/gst/fullpage.html?res=9C07E6D81538F933A25754C0A9669C8B63&sec=&spon=&pagewanted=2
  2. ^ http://www.beliefnet.com/author/author_145.html

Viungo vya nje hariri