John Eamon Gay (alizaliwa 7 Novemba 1996)[1] NI mwanariadha kutoka Kanada aliyebobea kwenye mbio za mwinuko za mita 3000. Mwaka 2019, alishindana kwenye mbio za mwinuko kwa wanaume kwenye michuano ya riadha ya mwaka 2019 yaliyofanyika Doha, Qatari[1]. Hakufuzu kushindana kwenye fainali

John Gay kwenye Olimpiki ya 2020
John Gay kwenye Olimpiki ya 2020

Mwaka 2017, alishiriki mbio ya mwinuko kwa wanaume ya mita 3000 kwenye 2017 Summer Universaide yaliyofanyika Taipei, Taiwan. [2]Alishikilia nafasi ya 11[2].

Mwaka 2019, alishindana kwenye senior men race kwenye michuano ya 2019 IAAF World Cross Country yaliyofanyika Aarhus, Denmarki[3]. Alishika nafasi ya 102.[3]

Mnamo Juni 2021, kwenye majaribio ya olimpiki Kanada, aliweka rekodi yake bora kwenye mita 3000 ya 8:20:68, huko Complexe Sportif Claude-Robillard, Montreal. Alishindana kwenye mbio za mwinuko za wanaume z amita 3000 kwenye michezo ya olimpiki majira ya joto ya 2020 yaliofanyika Tokyo, Japani.[4]

Marejeo hariri

  1. 1.0 1.1 0_Qsummary Mark (iaaf.org)
  2. 2.0 2.1 data.2017.gov.taipei
  3. 3.0 3.1 "Wayback Machine". web.archive.org. 2020-07-06. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-06. Iliwekwa mnamo 2021-10-13. 
  4. "Athletics GAY John - Tokyo 2020 Olympics". olympics.com (kwa en-us). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-08-28. Iliwekwa mnamo 2021-10-13.