John Michael Talbot

John Michael Talbot (amezaliwa tar. 8 Mei 1954 mjini Oklahoma City, Oklahoma) ni mfuasi wa Yesu Kristo, mwimbaji na mpigaji gitaa wa Kimarekani. Ni mwanzilishi wa The Brothers and Sisters of Charity huko Eureka Springs, Arkansas.[1]

John Michael Talbot
John Michael Talbot
Faili:JMTleft.jpg
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa John Michael Talbot
Amezaliwa 8 Mei 1954 (1954-05-08) (umri 70)
Asili yake Oklahoma City, Oklahoma, US
Aina ya muziki Christian;
Country Folk/Rock
Miaka ya kazi 1970's–hadi leo
Studio Sparrow Records (1970's–1996)
Troubadour for the Lord Records (1997–hadi leo)
Tovuti Little Portion Hermitage

Wasifu

hariri

Maisha y awali

hariri

Alizaliwa katika familia ya Wamethodist wenye historia ya muziki huko mjini Oklahoma City, Oklahoma. Aliamza kujifunza kupiga gitaa akiwa na umri wa miaka 10. Akiwa na umri wa miaka kumi na tano aliacha shule na akawa akifanyakazi kama mpiga gitaa wa Mason Proffit, bendi ya muziki wa rock/asili ilioanzishwa na kaka yake mkubwa, Terry. Bendi ilitoa albamu tano na ilikuwa moja kati ya bendi za muziki wa rock zilizopiga hatua na kupata mafanikio makubwa kama ilivyikubwa bendi ya Eagles


Baada ya kuvutwa karibu na kupata mafanikio, Talbot akajiingiza katika safari ya kiroho ambayo ilimwongoza mpaka katika dini za jadi za Kiamerika, Ubudha hadi Ukristo. Kwa maana hii yeye na ndugu yake wakajiunga katika Jesus Movement, wakarekodi albamu moja ilioitwa Reborn ambayo pia ilitoliewa tena na studio ya Sparrow Records(albamu asilia ilitolewa na jina la "The Talbot Bros." katika studio za Warner Brothers.

Baadaye albamu mbili za Talbot zilifuata: John Michael Talbot (1976) na The New Earth (1977). Albamu zote mbili zilitayarishwa na Billy Ray Hearn. Talbot alishawahi kuoa, kisha akaacha, na mkewe ndiye anayemlea binti yake. Baadaye akaamua kijtoa machoni mwa umma. Na kuanza kusoma maisha ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, alikuwa na shauku ya kuanza kusomea masula yake katika chuo cha Franciscan cha mjini Indianapolis.

Akawa Mromani Katoliki, na kujiunga na Secular Franciscan Order mnamo 1978. Baadaye akaanzisha nyumba ya ibada, The Little Portion, na akapanga kuishi maisha ya kujitenga (upweke). Baadaye ikatokea kuwa na maombi mengi yaliyokuwa yakiendele ya kiumuziki, Talbot akaendelea kutayarisha muziki wa sauti na gitaa katika staili ya Kiroma.


Alihamia kwenye Nyumba ya Ibada ya mjini Eureka Springs, Arkansas ambayo aliinunua wakati wa siku za Mason Proffit. Alianzisha jumuia yake mwenyewe ilioitwa Brothers and Sisters of Charity katika Little Portion Hermitage. Ni jumuia ambayo imejengwa kwa ajili ya watu aina mbalimbali, ikiwa na madada na makaka ambao hawajaolewa, vilevile na familia kadhaa.

Mnamo mwaka wa 1989, Talbot amemwoa (kwa ruhusa ya Kanisa la Katoliki) mwanamke mmoja aliyeitwa Viola Pratka, ambaye zamani alikuwa mwa wamoja wa "Incarnate Word Sister" (sista:mtawa; 'Incarnate Word Sister' enye oda ya Kikatoliki) ambaye alijiunga na jumuia hiyo mnam mwaka wa 1986. Kwa miaka mingi Talbot amesaidia sana shirika la Mercy Corp, shirika ambalo lanasaidia watu pale unapotokea msiba.

Mnamo mwaka wa 2008, Hermatige (Kiswahili: Kificho, ni jina la jumuia) ilisumbuliwa na tatizo la moto na kupelekea kuharibu maktaba zake na baadhi ya majengo mengine. Jumuia hiyo inaomba msaada kwa Mungu ili waweze kurejesha vile vitu vyote vilivyopotea kwenye ajali hiyo. Talbot ametumia muda wake mwingi sana kwa kwenda kudhuru eneo lile akiwa kama mtoa msaada-mwimbaji kwa ajili ya jumuia hiyo.

Albamu alizotoa

hariri
  1. Reborn (1972.)
  2. John Michael Talbot (1976.)
  3. The New Earth (1977.)
  4. The Lord's Supper (1979.)
  5. Beginnings / The Early Years (1980.)
  6. Come to the Quiet (1980.)
  7. The Painter (1980.)
  8. For the Bride (1981.)
  9. Troubadour of the Great King (1981.)
  10. Light Eternal (1982.)
  11. Songs For Worship Vol. 1 (1982.)
  12. No Longer Strangers (1983.)
  13. The God of Life (1984.)
  14. Songs For Worship Vol. 2 (1985.)
  15. The Quiet (1985.)
  16. Be Exalted (1986.)
  17. Empty Canvas (1986.)
  18. The Heart of the Shepherd (1987.)
  19. Quiet Reflections (1987.)
  20. The Regathering (1988.)
  21. Master Collection (1988.)
  22. The Lover and the Beloved (1989.)
  23. Come Worship the Lord Vol. 1 (1990.)
  24. Come Worship the Lord Vol. 2 (1990.)
  25. Hiding Place (1990.)
  26. The Birth of Jesus (1990.)
  27. The Master Musician (1992.)
  28. Meditations in the Spirit (1993.)
  29. Meditations from Solitude (1994.)
  30. Chant from the Hermitage (1995.)
  31. The John Michael Talbot Collection (1995.)
  32. The Talbot Brothers Collection (1995.)
  33. Brother to Brother (1996.)
  34. Our Blessing Cup (1996.)
  35. Troubadour for the Lord (1996.)
  36. Table of Plenty (1997.)
  37. Hidden Pathways (1998.)
  38. Pathways of the Shepherd (1998.)
  39. Pathways to Solitude (1998.)
  40. Pathways to Wisdom (1998.)
  41. Quiet Pathways (1998.)
  42. Spirit Pathways (1998.)
  43. Cave of the Heart (1999.)
  44. Simple Heart (2000.)
  45. Wisdom (2001.)
  46. Signatures (2003.)
  47. City of God (2005.)
  48. Monk Rock (2005.)
  49. The Beautiful City (2006.)
  50. Living Water 50th (2007.)
  51. Troubadour Years (2008.)

Marejo

hariri
  1. Simplicity (with Dan O'Neill) — (Troubadour For The Lord) ISBN 0-89283-635-0

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu John Michael Talbot kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.