Julian Huxley
Sir Julian Sorell Huxley (22 Juni 1887 – 14 Februari 1975) alikuwa mwanabiolojia na mwandishi kutoka nchi ya Uingereza. Anajulikana hasa kwa maandishi yake ya kisayansi aliyojaribu kuyafanya yaeleweke na watu wengi wa kawaida. Pia alikuwa mkurugenzi wa kwanza wa UNESCO. Alipewa cheo cha Sir cha Uingereza mwaka wa 1958.
Huxley alizaliwa ndani ya familia maarufu. Kwa mfano, kaka yake ni mwandishi Aldous Huxley, na kaka mwingine ni mwanabiolojia Andrew Huxley, mshindi wa Tuzo ya Nobel; baba yake ni mwandishi na mhariri Leonard Huxley. Tena, babu yake aliyemzaa mamake ni mwanabiolojia T. H. Huxley, aliyefanya kazi na kumsaidia Charles Darwin.
Viungo vya nje
haririWikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
- wasifu fupi Archived 4 Desemba 2004 at the Wayback Machine.
- Mwongozo wa insha za Huxley Archived 9 Julai 2007 at the Wayback Machine.
Insha
hariri- "Transhumanism" Archived 22 Mei 2011 at the Wayback Machine. katika: New Bottles for New Wine. London: Chatto & Windus, 1957.
- "The New Divination" Archived 11 Februari 2021 at the Wayback Machine. katika: Essays of a Humanist. London: Chatto & Windus, 1964.
Marejeo
hariri- Clark, Ronald, W. 1968. "The Huxleys". McGraw-Hill
- Huxley, J., 1957. "Transhumanism". Angalia kiungo cha insha hiyo huko juu.
- Huxley, J., 1970. Memories. George Allen & Unwin, London.
- Kevles, D. J., 1985. In The Name Of Eugenics. University of California Press.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Julian Huxley kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |