Juliana Kanyomozi

Juliana Kanyomozi (anajulikana sana kwa jina lake la kwanza Juliana; amezaliwa 27 Novemba 1981) ni msanii wa kike kutoka Uganda ambaye ameimba nyimbo kama Say yes (Sema Ndiyo), Nabikoowa, Diana (hayati Philly Lutaaya) na Nkulinze.

Pia amefanya kazi na Bobi Wine kwenye nyimbo Taata Wa Banna Yanni (Nani ndiye baba wa watoto) na Mama Mbiire.

Yeye alikuwa mtangazaji wa kipindi cha asubuhi katika kituo cha redio cha Capital FM mjini Kampala.

Pia ametoa wimbo na mwimbaji wa Tanzania Bushoke (Usiende Mbali). na alitozwa taji la Uganda's Fashion icon mwaka 2008.

TuzoEdit

Alishinda:

  • 2004 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) - Msanii bora katika kitengo cha R & B[1]
  • 2005 Pearl of Africa Music Awards - Wasanii bora katika kitengo R & B na Msanii bora wa kike na Wimbo wa Mwaka ( "Mama Mbiire" na Bobi Wine) pia Wimbo bora katika kitengo cha R & B ( "Nabikowa") [2]
  • 2007 Pearl of Africa Music Awards - Msanii/kikundi bora katika kitengo cha mziki wa R & B [3]
  • 2008 Pearl of Africa Music Awards - Msanii wa Mwaka & msanii bora katika R & B & Msanii bora wa kike[4]

Ameteuliwa:

MarejeoEdit

  1. [4] ^ PAM Awards: Washindi wa 2004
  2. PAM Awards: 2005 Winners
  3. Museke: Pearl of Africa Music (PAM) Awards 2007 Washindi - Uganda Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
  4. Museke: Pearl of Africa Music (PAM) Awards 2008 Washindi - Uganda Archived 5 Juni 2015 at the Wayback Machine.
  5. [9] ^ Kisima Awards: Nominees 2008

Viungo vya njeEdit