Bobi Wine

Mwanasiasa,muigizaji,mwanamuziki na mwanaharakati wa Uganda

Robert Kyagulanyi Ssentamu (anajulikana kwa jina la kisanii kama Bobi Wine; alizaliwa 12 Februari 1982) ni mwanasiasa, mwimbaji, mwigizaji na mfanyabiashara wa Uganda.[1] ni kiongozi katika harakati maarufu dhidi ya Rais Yoweri Museveni na harakati hizo hujulikana kama People Power, Our Power.[2] mwaka 2019, alitangazwa kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa Uganda.

Bobi Wine mwaka 2019.

Kyagulanyi alizaliwa katika hospitali ya Nkozi, ambapo mama yake aliwahi kufanya kazi.[3] alikulia katika mji mkuu wa Uganda Kampala .[4]

Kyagulanyi alisoma katika shule ya Kitante Hill School, ambapo alipata cheti cha elimu yake ya msingi mwaka 1996. Mwaka 1998 alihitimu elimu ya upili katika shule ya Kololo Senior Secondary School na kupata cheti, kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere alikosomea muziki na sanaa ambapo alihitimu kwa ngazi ya diploma mwaka 2003, mnamo mwaka 2016 Kyagulanyi alirudi tena chuo kikuu na kujifunza sheria katika International University of East Africa (IUEA).

Marejeo hariri

  1. Editor. Bobi Wine Biography, Early Life, Age, Family, Education, Career And Net Worth.
  2. URN. "Can 'People Power' change Uganda's political fortune?", The Observer - Uganda. (en-gb) 
  3. Mazinga, Mathias (14 June 2016). Cardinal Wamala, singer Bobi Wine set for Nkozi Hospital marathon. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-01-19.
  4. Ariba, Caroline (6 September 2012). Bobi giving back to the hands that lifted him up. Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-01-10. Iliwekwa mnamo 2021-01-19.
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Bobi Wine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.