Jumanne Kibera Kishimba

Jumanne Kibera Kishimba ni mwanasiasa Mtanzania na mwanachama wa chama cha kisiasa cha CCM. Amekuwa mwanachama hai wa CCM tangu 1996. Alishinda ubunge kwa tiketi ya chama hicho kwa miaka 20152020. [1]

Jumanne Kishimba amekuwa maarufu Tanzania kutokana na kuwa na hoja za pekee ambazo huonekana kuwa ni hoja nyepesi na ambazo mara nyingi huibua mijadala hasa kuhusu elimu, biashara na malezi pamoja na masuala ya dini na imani. Hoja zake nyingi zimejikita katika kukosoa mitazamo ya wasomi na wanasiasa wa Tanzania katika ufanyaji wa maamuzi bila kutazama hali za watanzania na changamoto wanazokutana nazo.

Moja ya hoja yake maarufu ilihusu kitenda cha muda unaotumika katika elimu ambapo kwa wastani mtoto wa Kitanzania husoma kwa zaidi ya miaka 17 na kisha hurejeshwa nyumbani na kuambiwa ajiajiri kwa sababu serikali na sekta binafsi nchini Tanzania hazina ajira. Yeye anajulikana kwa kuhoji kwamba elimu hiyo wanayopewa katika kipindi chote haiwajengi kuweza kujiajiri katika shughuli zao za kawaida kama kilimo na ufugaji na hivyo kujikuta wakiwa hawana stadi za maisha.

Eneo lingine ambalo mbunge huyu amefahamika kwa kukosoa ni suala la mitihani, kukatazwa kwa matumizi ya mabati ya bei chini na tofali za kuchoma huku asililimia kubwa ya wakazi wa Tanzania wakiishi katika nyumba zilizoezekwa kwa nyasi na matembe.

Kishimba ni mkurugenzi wa kampuni ya IMALASEKO supermarket ambayo ni moja ya kampuni zenye maduka makubwa ya bidhaa anuai katika jiji la Dar es Salaam na kwingineko Tanzania.

Marejeo

hariri
  1. Tovuti ya Bunge la Tanzania, iliangaliwa Mei 2017