Chama cha Mapinduzi

(Elekezwa kutoka CCM)

Chama cha Mapinduzi (CCM) ni chama tawala nchini Tanzania.

Historia

CCM ilizaliwa tarehe 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama tawala cha Zanzibar wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.

Itikadi

 
CCM kina wafuasi wengi vijijini.

Kwa miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha.

Kutokana na azimio hilo uchumi uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.

Uchaguzi

CCM imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa nchini Tanzania.

Chama hicho kimekuwa pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi, ingawa vyama vya upinzani vilitoa malalamiko kuhusu utekelezaji wa haki na uchakachuaji wa kura.

Chaguzi za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 na viongozi walioweza kuwa washindi kakati chama hicho ni kama wafuatao: Benjamin Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete. Hawa ndio viongozi waliongoza nchi kipindi cha miaka ishirini.

Katika historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti watano:

Viungo vya nje