Kabonati
Kabonati (kutoka Kiingereza carbonate) ni kampaundi yoyote yenye ioni ya CO32-. Ioni hiyo inafanywa na kaboni na oksijeni.
Kabonati hutokea kama chumvi na esta za asidi kabonia (H2CO3 carbonic acid).
Kabonati zinapatikana kote katika mazingira yetu, hasa katika miamba kwa mfano gange. Viumbehai wengi wana viunzi vinavyofanywa na kabonati, hasa chokaa.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kabonati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |