Gange au mawe chokaa (ing. limestone) ni aina ya mwamba mashapo inayotokana na madini ya kalsiti (calcite) inayofanywa na kabonati ya kalisi CaCO3.[1]

Mfano wa Gange
Mfano wa Gange huko Provo Canyon, Utah
Mfano wa Gange zikitumika kama kifaa cha ujenzi

Kabonati ya kalisi inatengenzwa na viumbehai vinavyojenga kiunzi cha kujikinga au kuimarisha miili yao, kama kiunzi cha matumbawe au sifonji, lakini pia kiunzi cha mifupa ya wanyama wakubwa. Matumbawe hujenga matabaka manene ya mwamba chokaa, mabaki ya viumbe vingine katika maji hutiririka chini ambako yanajenga matabaka ya kalsiti inayokandamizwa na shinikizo ya mata inayokaa juu yake, jinsi ilivyo na mwamba mashapo wote.

Matabaka ya gange yalitokea chini ya bahari katika muda wa kiaka mamilioni hata mabilioni. Yalikua hadi kuwa na unene wa kilomita kadhaa. Gange ni takriban silimia 10 ya miamba mashapo yote duniani.

Pale ambako gange iliathiriwa na joto na shinikizo kubwa sana imebadilika kuwa mwamba metamofia, kwa mfano marumaru.

Gange ni muhimu sana kwa jamii za binadamu kama kifaa cha ujenzi. Gange si ngumu mno hivi iliwahi kukatwa tangu miaka mielfu na kutumiwa kwa majengo. Piramidi za Misri zilijengwa kwa kutumia gange.

Saruji inatengenezwa kwa kuchoma gange.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gange kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.