Kampuni ya Green Bus Lines
Green Bus Lines ilikuwa kampuni ya mabasi katika jiji la New York,Marekani.Ilisimamiwa na hivi majuzi kabisa na Bw.Jerome Cooper(mwana wa marehemu mwanzilishi/mmiliki Bw. William Cooper 1895 - 1985) na ikaendesha biashara zake katika mitaa ya Queens na pia kuwa na mabasi ya kuenda hadi Manhattan bila kusimama.Ilifanya hivi hadi 9 Januari 2006,ndipo Kampuni ya MTA ilichukua njia maalum za Green Bus Lines.
Kampuni hii ilianzishwa 3 Aprili 1925 ili kuwasilisha huduma ya mabasi katika mitaa. Mabasi yake yalikuwa yakipitia njia nyingi maalum za Manhattan(hizi zinahusisha njia za sasa M22, M27, M50, M79, M86 na M96) katika mwaka 1933,lakini mamlaka za kutumia njia hizi zikapewa Shirika la Comprehensive Omnibus katika mwaka wa 1935 na Shirika la New York City Omnibus katika mwaka wa 1936, na Green ikanunua mamlaka za njia zingine za upande wa kusini mashariki mwa Queens. Green ilinunua pia mashirika ya mabasi ya Manhattan na Queens,iliyokuwa inaendesha mabasi ya Manhattan and Queens Traction Company Queens Boulevard hapo awali huko Manhattan tangu 1937, katika mwaka wa 1943.
Green ilinunua kampuni zingine kadhaa zilizoendelea kujiendesha zenyewe,hasa: Kampuni ya Command Bus, Shirika la Triboro Coach, na Mabasi ya Jamaika.
QM23 za kisasa zilianzishwa katika miaka ya 1950 ili kuchukua nafasi ya huduma za reli ya Long Island hadi kwa stesheni ya Brooklyn Manor karibu natawi la Rockaway Beach. Njia nne zaidi za kufika maeneo mbalimbali bila kusimama njiani zilianza operesheni katika miaka ya 1950.
Njia zilizotumiwa na mabasi ya Green Bus
haririKabla ya kununuliwa na Kampuni ya MTA, Green Bus ilikuwa ikiendesha mabasi yake katika zifuatazo,nyingi zikiwa na makao maalum katika Vituo vya Basi vya Far Rockaway na John F Kennedy.
Njia Katika Mtaa wa Queens
hariri- Q6 Sutphin Boulevard
- Q7 Rockaway Boulevard na Pitkin Av
- Q8 101 Avenue
- Q9 Lincoln Street
- Q10 Lefferts Boulevard na Rockaway Blvd / Hasa karibu na vituo vya Uwanja Kuu wa Ndege wa JFK
- Q11 Woodhaven Boulevard
- Q21 Cross Bay Boulevard
- Q22 Rockaway Beach
- Q35 Newport Avenue na Flatbush Avenue (Brooklyn)
- Q37 111th Street
- Q40 142 Street
- Q41 127 Street
- Q60 Queens Boulevard
- Q89 (Hapo zamani illitwa Q9A) Linden Boulevard na Lincoln Street
Njia za kusafiri bila kusimama njiani
hariri- QM15 Midtown Manhattan - Lindenwood
- QM16 Midtown Manhattan - Rockaway Park
- QM17 Midtown Manhattan - Far Rockaway
- QM18 Midtown Manhattan - South Ozone Park, ikipitia Lefferts
- QM23 Midtown Manhattan - Brooklyn Manor