Usafiri ni uhamisho wa watu au vitu na bidhaa kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine.

Treni ya Shinkansen nchini Japani.
Feri kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Ndege ya Boeing 747-300.

Usafiri unakuja pamoja na muundombinu kama njia za usafiri, vyombo vya usafiri na wahusika wake kama makampuni, shirika na abiria.

Njia za usafiri

Njia za usafiri hutofautishwa kufuatana na aina yake kama ni:

Vyombo vya usafiri

Vyombo vya usafiri hulingana na njia zinazotumika.

Usafiri wa nchi kavu hutumia motokaa, treni, baisikeli au pikipiki.

Usafiri wa majini hutumia meli, boti, jahazi na mengine.

Usafiri wa hewani hutumia ndege, helikopta au ndegeputo[1].

Faida ya usafiri

  • Husaidia katika kufikisha haraka vyakula au matunda yanayooza mapema.
  • Husaidia kufikisha haraka habari zilizo kwenye majarida n.k.
  • Huwezesha mahusiano kati ya nchi na nchi.
  • Husaidia biashara za masafa marefu kuendelea.
  • Pia husaidia katika maendeleo ya nchi (kimapato)

Tanbihi