Kampuni ya Viatu ya Brown

Kampuni ya Viatu ya Brown [1] ni kampuni ya viatu ambayo inamiliki aina mbalimbali ya viatu nchini Marekani na Kanada. Makao yake makuu yanapatikana Clayton, Missouri ,kitongoji kidogo kilichokuwa karibu na St. Louis, Missouri.

Kampuni ya Viatu ya Brown
Jina la kampuni Kampuni ya Viatu ya Brown
Mwanzilishi George Warren Brown
Alvin Bryan
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji
Makao Makuu ya kampuni Clayton,Missouri
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu
Nchi Marekani
Tovuti http://www.brownshoe.com/
Buster Brown na Tige wamewakilisha kampuni ya Brown kwa miaka mingi tangu 1904

Asili ya kampuni

hariri

Kampuni hii ilianzishwa katika eneo la St. Louis na hapo awali iliitwa Bryan, Brown & Company kwa makumbusho ya waanzilishi George Warren Brown na Alvin Bryan. Jina lilibadilishwa kuwa Kampuni ya Viatu ya Brown katika mwaka wa 1893. Shule ya George Warren Brown ya Kazi kwa Jamii ilianzishwa katika Chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis katika mwaka wa 1925 na mjane wake GW Brown.

Uendeshaji wa biashara.

hariri

Kampuni ya Viatu ya Brown, ni kampuni ya thamani ya $ bilioni 2.4 ikiwa na operesheni zake kote duniani. Kampuni hii inaendesha mnyororo wa maduka 1100 ya Famous Footwear. Inaendesha ,pia, maduka 300 maalum ya rejareja nchini Marekani, Uchina na Kanada chini ya majina kama Brown Shoe Closet, FX LaSalle , Franco Sarto na ,pia, Shoes.com (tovuti rasmi ya kibiashara ya kampuni). Sehemu za kampuni hii za kuuza bidhaa kwa wingi na ,pia, zenye viatu maarufu ni kama Naturalizer, LifeStride, Via Spiga, Nickels Soft, Connie na Buster Brown. Kampuni hii ina leseni ,pia, ya uuzaji wa viatu vinavyojulikana sana vya watu wazima kama Franco Sarto, Etienne Aigner, Dr. Scholl's, Carlos ya Carlos Santana na Fergie. Vilevile, inauza viatu vya watoto vya Barbie na Nickelodeon.

Katuni za kuwakilisha kampuni

hariri

Tangu mwaka wa 1904, katuni za kuwakilisha kampuni zimekuwa Buster Brown na mbwa wake, Tige(angalia picha kule juu). Wote wawili huonekana kwenye matangazo ya televisheni ya kampuni. Katika miaka ya 1940 na 1950, kampuni iliingia ,kwa muda mfupi, katika uchapishaji wa magazeti yenye michoro ya katuni. Magazeti haya yalihusisha katuni maarufu Buster Brown kwenye ukurasa wa kwanza ingawa hekaya zingine pia zilichorwa katika machapisho haya, kama zile za Robin Hood.

Marejeo

hariri
  1. ^ "Clayton city, Missouri." Ilihifadhiwa 6 Septemba 2009 kwenye Wayback Machine. U.S. Census Bureau.
  2. ^ "We're Brown Shoe." Brown Shoe Company.

Viungo vya nje

hariri