Kampuni ya Viatu ya Goodwill

Kampuni ya Viatu ya Goodwill (pia, hujulikana kama Viatu vya Arthur A. Williams, likiitwa jina hili kwa makumbusho ya mwanzilishi wake). Kampuni hii huunda viatu vya ngozi na vya kutiwa chuma ndani vya aina ya "Safety First" (yaani vya kujichunga kutokana na kujiumiza).Kampuni hii ilikuwa miongoni mwa kampuni za kwanza kuunda viatu vya aina hii. Haswa, ilikuwa mojawapo wa kampuni kubwa kabisa zilizounda buti za viwanda katika miaka ya 1930. Kampuni hii ilitumbukia katika dimbwi la madeni hapo katikati mwa karne ya ishirini.

Kampuni ya Viatu ya Goodwill
Jina la kampuni Kampuni ya Viatu ya Goodwill
Ilianzishwa 1909, Massachusetts
Mwanzilishi Arthur A. Williams
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji
Makao Makuu ya kampuni 26-28 Water Street Holliston,Massachusetts
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu kama:
* buti
* viatu vya ngozi
Nchi Marekani
mkebe wa kihifadhi viatu mapema karne ya 20

Kiwanda cha Kampuni ya Viatu ya Goodwill(kilichojengwa katika mwaka wa 1909), kinapatikana katika barabara ya 26-28 Water Street Holliston,Massachusetts.

"Huu ni mfano wa kihistoria wa kiwanda kikubwa cha maonyesho kilichojengwa katika kilele cha ujenzi katika sekta ya viwanda vya maonyesho. Kiwanda hiki kilijengwa kwa faida ya utengenezaji wa viatu vizito vya wakulima na wanamichezo. Majengo yao mawili ya mbao yanapatikana katika pande mbili zote za barabara ya Water Street na yalikuwa yameunganishwa kwa daraja katika gorofa la pili na lilipita juu ya barabara hiyo. Vilevile,kulikuwa na njia ya kupitia iliyokuwa chini ya ardhi ya barabara ya Water Street. Jengo lililokuwa katika upande wa mashariki wa barabara hii lilikuwa la magorofa manne , upana wa futi 190 na mnara ambao ulikuwa na paa ya sleti.Jengo lililokuwa katika upande wa magharibi lilikuwa la magorofa matatu na upana wa futi 10. Majengo yote yanaonyesha mabango yao ya hapo awali yaliyokuwa na alama za 6/6." Hii ni ripoti ya Idara ya Ndani ambayo ni muhtasari ikieleza vizuri kuhusu majengo hayo. Mwandishi wa makala haya ni Monica E. Hawley,mwanahistoria.

Marejeo hariri