Kanda Bongo Man
Kanda Bongo Man, alizaliwa mwaka wa 1955 huko Inongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni mwanamuziki maarufu wa soukous.[1]
Kanda Bongo Man alikuwa mwimbaji wa Orchestra Belle Mambo mwaka wa 1973, kuendeleza sauti iliyopendekezwa na Tabu Ley [2] Wasifu wake binafsi ulianza baada ya kuhamia Paris mwaka 1979 ambapo muziki wake ulianza kuingiza vipengele vya muziki wa Zouk (asili yake ni Kifaransa katika West Indies). Albamu zake za kwanza , "Iyole" mwaka 1981 na "Djessy" mwaka 1982 zilivuma.
Yeye ni mashuhuri zaidi kwa mabadiliko katika muziki wa soukous. Mkabala uliopita ulihusu kuimba mistari kadhaa na kupiga gitaa ifikapo mwisho wa wimbo. Kanda Bongo Man alirembesha soukous na kwa kuhimiza utumiaji wa gitaa baada ya kila mstari na hata wakati mwingine katika mwanzo wa wimbo. Mtindo wake wa soukous ulisababisha densi ya kwassa kwassa ambapo nyonga inasongs nyuma na mbele wakati mikono inafuata nyonga.
Kama wengi wa wanamuziki soukous na rumba kutoka Afrika waliokuwa mbele yake, Kanda Bongo Man pia alikuwa na kundi la wanamuziki alioimba nao. Wengi wa wanamuziki wa Kanda baadaye walihama na kuanza kuimba binafsi. Aliyejulikana sana ni Diblo Dibala. Akijulikana k kama "Machine Gun", Diblo Dibala alikuwa sehemu muhimu katika kundi la Bongo Man'katika Albamu kadhaa pamoja na "Kwasa Kwasa" na "Amour Fou".
Kanda Bongo Man bado anazuru Ulaya na Marekani. Julaimwaka wa 2005 aliimba katiak LIVE 8: Onyesho la Afrika katika Cornwall.
Diskografia
hariri- Iyole (1981)
- Djessy (1982)
- Amour Fou (1984)
- Malinga (1986)
- Lela Lela (1987)
- Sai Liza (1988)
- Kwassa Kwassa (1989)
- Isambe Monie (1990)
- Zing Zong (1991)
- Sango (1992)
- Soukous katika Central Park (1993)
- Tamu (1995)
- Karibu Afrika Kusini (1995)
- Francophonix (1999)
- Balobi (2002)
- Swalati (2003)
- (2009)
Viungo vya nje
hariri- Soukous.com Biografia ya Kanda
- Tovuti Rasmi Ilihifadhiwa 2 Desemba 2006 kwenye Wayback Machine.
- Kumbukumbu ya muziki kutoka Afrika: Kanda Bongo Man Ilihifadhiwa 31 Mei 2008 kwenye Wayback Machine.
Tanbihi
hariri- ↑ "African Music Encyclopedia: Kanda Bongo Man". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-31. Iliwekwa mnamo 2010-01-02.
- ↑ Chris Stapleton's sleevenotes kwa Heartbeat Soukous