Kanisa kuu la kujifunza

Kanisa kuu la kujifunza (Cathedral of Learning kwa Kiingereza) ni jengo la kitaaluma katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh jimbo la Pennsylvania nchi ya Marekani. Kanisa kuu liko katikati ya chuo cha Oakland.  Ni jengo la elimu refu zaidi katika nusu ya magharibi ya dunia. Pia, ni jengo la pili la Kigothi refu zaidi duniani. Kuna ghorofa arobaini na mbili, na kanisa kuu lina urefu wa futi mia tano thelathini na tano. Ujenzi ulianza mwaka elfu moja mia tisa ishirini na sita. Madarasa yalianza mwaka elfu moja mia tisa thelathini na moja, lakini Kanisa kuu lilimalizwa mwaka elfu moja mia tisa thelathini na nne. Ni jenga muhimu kwa mji wa Pittsburgh. [1]

Kanisa kuu la kujifunza

Sasa, Kanisa kuu la kujifunza ni katikati ya maisha ya wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh. Wanafunzi wengi wanaliita kanisa kuu “Cathy,” na kuna zaidi ya elfu mbili vyumba na madirisha. Ndani ya kanisa kuu kuna ofisi nyingi za idara za chuo kikuu na pahali muhimu kama uwanja wa maonyesho, kantini, nafasi za masomo, maabara za kompyuta na lugha, na mgahawa wa kahawa. Kanisa kuu la kujifunza linajulikana kwa vyumba vya utaifa. Kuna vyumba vya utaifa thelathini na moja ndani ya Kanisa kuu la kujifunza, na kila chumba ni kwa heshima ya taifa moja na utamaduni wake.

Vyumba vya utaifa hariri

Kanisa Kuu la kujifunza lina vyumba vya utaifa thelathini na moja, na ishirini na tisa vya hivyo vinaweza kuwa na madarasa. Viwili vya vyumba vinatumiwa kwa pambo tu. Kila chumba kinapambwa kwa kuonyesha utamaduni wa taifa wake. Programu ya vyumba vya utaifa ilianza mwaka elfu moja mia tisa ishirini na sita kwa sababu John Bowman, Mkuu wa kumi wa Chuo Kikuu, alitaka kwamba jumuia ya Pittsburgh imehusika na Kanisa Kuu, kwa hivyo kila utaifa na watu wengi katika mji wa Pittsburgh wangeweza kujenga chumba. Kila chumba kilikuwa dola laki tatu au zaidi kwa kujenga. Vyumba vipya vimekuwa pesa zaidi.                    

 
Chumba cha utaifa cha Kiafrika

Kila chumba kina kamati ambayo inachora chumba na inachangisha pesa kwa kujenga na kuendeleza chumba. Chuo Kikuu kinatoa nafasi kwa chumba, lakini kamati anahitaji kupata pesa. Mara kwa mara, serikali za mataifa zinatoa pesa ili kujenga vyumba vyao. Leo, kamati za vyumba vya utaifa zinahitaji kuwatoa pesa kwa wanafunzi kwa hivyo wanaweza kusafiri wakati wa majira ya kiangazi.

Idara ya digrii ya daraja la juu hariri

 
Dirisha kutoka ghorofa la 36 katika Kanisa kuu cha kujifunza

Idara ya digrii ya daraja la juu iko Kanisa Kikuu la Kujifunza katika ghorofa la thelathini na sita. Idara ilianza mwaka elfu moja mia moja themanini na sita. Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Pittsburgh wanaweza kupata digrii ya daraja la juu kama “BPhil” au wanaweza kupata pesa kwa kusoma. Mwaka elfu mbili ishirini na mbili David C. Frederick alipa msaada mkubwa sana ili kukuza programu.      

  1. "Cathedral of Learning | Campus Tour". www.tour.pitt.edu. Iliwekwa mnamo 2023-12-12.