Karne ni muda wa miaka mia moja. Karne 10 ni milenia moja. Inawezekana kugawa karne kwa miongo 10.

Neno hili limetokana na Kiarabu "ﻗﺮﻥ" linamaanisha kipindi cha miaka mia moja. Kwa kawaida karne si miaka 100 yoyote inayofuatana lakini kipindi kati ya miaka kama vile 1901-2000 au 1801-1900.

Karne inakwisha katika mwaka wenye "00" mwishoni yaani 1700, 1800, 1900, 2000. Sababu yake ni kwamba hakuna mwaka "0" ya kuanzisha hesabu, hivyo karne ya kwanza ya hesabu ilianza kwa mwaka 1. Hali hii huleta kila karne majadiliano kwa sababu watu wengi husikia karne mpya inaanza wakati tarakimu ya mbele waliyozoea muda mrefu inabadilika.

Hivyo watu wengi walisheherekea karne mpya mwanzoni wa mwaka 2000 iliyokuwa mwaka wa mwisho wa karne ya 20, si mwaka wa kwanza wa karne ya 21. Ingawa maoni ya wataalamu hayakueleweka au hayakupokelewa, watu wengine walisema haidhuru.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Karne kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.