Kasese ni mji mkuu wa Wilaya ya Kasese nchini Uganda wenye wakazi wake takriban 66,600. Mji uko magharibi mwa Ziwa George. Awali mji huu ulikua kutokana na uchimbaji wa madini ya shaba katika eneo ka Kilembe, na hapo baadaye uchimbaji wa kobalti. Huu ndio mji mkuu wa Wilaya ya Kasese na makao makuu ya wilaya yapo hapo. Kasese pia ndio mji mkubwa kwenye Mkoa wa Rwenzururu. Makazi ya Charles Mumbere, Omusinga wa Rwenzururu yako katika mji huu.

Mji wa Kasese
Kasese
Kasese is located in Uganda
Kasese
Kasese
Mahali pa mji wa Kasese katika Uganda
Majiranukta: 0°11′12″N 30°05′17″E / 0.18667°N 30.08806°E / 0.18667; 30.08806
Nchi Uganda
Mkoa Magharibi
Wilaya Kasese
Idadi ya wakazi
 - 66,600

LocationEdit

Kasese ni mji ulioko sehemu ya mwisho kabisa ya Reli ya Uganda upande wa magharibi inyoelekea Kampala na Tororo na pia ndipo ulipo Uwanja wa Ndege wa Kasese. Mji uko jirani na Milima ya Rwenzori na Mbuga ya Kitaifa ya Queen Elizabeth.

Idadi ya wakazɪEdit

 
Old Kasese Train Station

Agosti 2014, Uganda Bureau of Statistics ilikaridia kuwa Kasese ina wakazi wapatao 101,679.[1] Kasese ni kati ya miji inayokua kwa kasi zaidi nchini Uganda.

VivutioEdit

 
Kilembe Copper Mine

Vivutio hivi vimo katika mji huu na pembezoni mwake:

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  1. UBOS (27 August 2014). The Population of The Regions of the Republic of Uganda And All Cities And Towns of More Than 15,000 Inhabitants. Citypopulation.de Quoting Uganda Bureau of Statistics (UBOS). Iliwekwa mnamo 22 February 2015.
  2. Asiimwe, Wilson (7 June 2014). Kilembe mines rehabilitation starts. New Vision. Iliwekwa mnamo 13 September 2015.
  3. Enid Ninsiima, and Thembo Kahungu Misairi (13 September 2015). Four killed as floods sweep Kilembe Mines hospital. Iliwekwa mnamo 1 July 2015.
  4. Thawite, John (4 June 2013). Kilembe Hospital re-opens. Iliwekwa mnamo 13 September 2015.
  5. John Thawite, and Taddeo Bwambale (8 May 2014). Five perish as fresh floods hit Kasese. Iliwekwa mnamo 13 September 2015.

Viungo vya njeEdit

  Kasese travel guide kutoka Wikisafiri

Wikimedia Commons ina media kuhusu: